-
Waziri wa Ulinzi asisitiza kuongezwa uwezo wa jeshi la majini la Iran kulingana na ukubwa wa vitisho
Jun 19, 2022 05:45Akiwa ziarani katika mkoa wa Hormozgan kusini mwa Iran, Brigedia Jenerali Mohammad Reza Ashtiani, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametembelea miradi ya majini ya wizara hiyo huko Bandar Abbas hususan utengenezaji wa manowari, meli za kawaida za kivita na nyambizi na kusema kuwa kuimarishwa nguvu katika pande zote za ulinzi ikiwa ni pamoja na nchi kavu anga, na hasa baharini, ni moja ya vipaumbele vya mipango ya ulinzi wa nchi.
-
Iran: Ushirikiano wa kieneo ndio utaimarisha usalama Ghuba ya Uajemi
Apr 15, 2022 04:01Waziri wa Ulinzi wa Iran amelaani uwepo haramu wa madola ajinabi katika eneo la kistratajia la Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormuz na kusisitiza kuwa, ushirikiano wa nchi za Asia Magharibi ndiyo dawa mjarabu ya kudhamini usalama na uthabiti wa eneo hili.
-
Mazungumzo baina ya Iran na Oman kuhusu usalama wa baharini
Mar 10, 2022 04:10Kikao cha Tatu cha Makamanda wa Gadi ya Ufukweni ya Jamhuri ya Kiisalmu ya Iran na Oman kimefanyika mjini Muscat na kujadili usalama wa baharini. Maudhui kuu iliyojadiliwa na nchi hizi mbili ndugu katika kikao hicho ni kuzidi kushirikiana na kuwa na uratibu wa pamoja na kulinda usalama wa mpaka wa baharini wa nchi hizo.
-
Iran: Uhusiano wetu na Oman ni wa jadi na imara sana
Jan 10, 2022 14:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa, uhusiano wa Tehran na Oman ni wa jadi na imara na kwamba siasa za serikali ya Iran zitaendelea kuwa za kupigania uhusiano imara na majirani zake.
-
Safari ya Zarif katika nchi za eneo; ujumbe wa kudhamini usalama wa eneo kupitia mpango wa "Amani ya Hormuz"
May 01, 2021 02:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif amefanya safari katika nchi za eneo hili la Ghuba ya Uajemi, ambapo kwa kuanzia alielekea Qatar na kisha akazitembelea Iraq, Oman na Kuwait; ajenda kuu ya mazungumzo yake na viongozi wa nchi hizo ikiwa ni kubadilishana mawazo kuhusu namna ya kustawisha uhusiano wa pande mbili, pamoja na kujenga ushirikiano wa pamoja wa kudhamini amani na usalama wa eneo hili.
-
Iran: Tunafuatilia kwa karibu nyendo za Marekani katika Ghuba ya Uajemi
Jan 04, 2021 15:48Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema Tehran inafuatilia kwa jicho la karibu nyendo na harakati za kutilia shaka za Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
-
Kuwait: Jukumu la usalama wa Ghuba ya Uajemi ni la nchi zote za eneo hilo
Dec 15, 2020 11:34Waziri Mkuu wa Kuwait amesema kuwa, suala la kulinda usalama wa Ghuba ya Uajemi ni jukumu la nchi zote za eneo hilo na hakuna nchi yoyote inayoweza kujivua na jukumu hilo.
-
Kupasishwa na Seneti ya Marekani uamuzi wa kuiuzia silaha za kisasa Imarati
Dec 11, 2020 02:56Marekani daima imekuwa ikitumia porojo kulioonesha eneo la Asia Magharibi kwamba, linakabiliwa na ukosefu wa amani na kueneza chuki dhidi ya Iran sambamba na kuionyesa mbele ya macho ya mataifa ya eneo hili kwamba, ni tishio ili kwa njia hiyo ijiandalie uwanja wa kuziuzia silaha nchi za Ukanda wa kusini mwa Ghuba ya Uajemi.
-
Jumamosi, 28 Novemba, 2020
Nov 28, 2020 03:26Leo ni Jumamosi tarehe 12 Mfunguo Saba Rabiu Thani 1442 Hijria ambayo inasadifiana na tarehe 28 Novemba 2020 Miladia.
-
Meja Jenerali Salami: Ghuba ya Uajemi ni ngome imara ya kujilinda Iran ya Kiislamu
Nov 19, 2020 11:15Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Ghuba ya Uajemi ni ukanda wenye nguvu wa kuilinda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni makutano ya makabilianao baina ya madola.