-
Iran: Tutatoa jibu madhubuti kwa vitisho vya Israel
Sep 15, 2023 08:25Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu itatoa jibu madhubuti kwa vitisho vyovyote na vitendo haramu vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya taifa hili.
-
Raisi: Ukraine haijawasilisha ushahidi wa madai ya kutumwa silaha za Iran kwa Russia wakati wa vita
Sep 14, 2023 07:43Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waukraine wameshindwa kuwasilisha nyaraka zozote zinazoonyesha kuwa, Jamhuri ya Kiislamu iliipatia silaha Russia wakati wa vita.
-
Ebrahim Raisi: Iran imethibitisha kuwa ni rafiki wa Iraq katika nyakati ngumu
Sep 14, 2023 04:09Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijawahi kusita kutoa msaada wowote kwa ajili ya kuihami Iraq katika vita dhidi ya magaidi wa Daesh (ISIS) na imethibitisha kivitendo kuwa ni rafiki mwaminifu wa Iraq katika nyakati ngumu.
-
Spika wa Bunge la Iran aelezea masikitiko yake kwa serikali na watu wa Libya baada ya mafuriko
Sep 13, 2023 23:25Katika ujumbe wake kwa Spika mwezake wa Bunge la Libya, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameelezea masikitiko yake kwa serikali na wananchi wa Libya kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
-
Rais wa Iran atuma salamu za rambirambi kwa taifa Libya kufuatia maafa ya mafuriko
Sep 12, 2023 10:44Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma salamu za rambirambi kwa Waziri Mkuu na wananchi wa Libya kutokana na vifo vya maelfu ya watu nchini huko vilivyosababishwa na Kimbunga Daniel kilichoikumba nchi hiyo na kuzusha mafuriko makubwa.
-
'Wadukuzi wa Iran' wapenya kwenye mitandao ya makampuni zaidi ya 30 ya Israel
Sep 12, 2023 02:58Tovuti ya Israel ya Ynetnews imeripoti kuwa wadukuzi wa Iran wamefanikiwa kupenya kwenye mitandao ya makampuni zaidi ya 30 ndani ya utawala huo haramu wa Kizayuni.
-
Iran yasikitishwa na zilzala iliyoua maelfu Morocco; kutuma nchini humo misaada ya kibinadamu
Sep 10, 2023 07:25Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo tayari kutuma misaada ya kibinadamu nchini Morocco, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoua maelfu ya watu.
-
Iran kuunda makombora mapya ya hypersonic kuikabili Israel
Sep 10, 2023 07:08Kamanda wa ngazi ya juu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amefichua mpango wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuunda makombora mapya ya hypersonic ambayo anasisitiza kuwa yataufanya utawala wa Kizayuni ulipe gharama kubwa.
-
Mahudhurio ya kwanza rasmi ya Iran katika kikao cha Baraza la Kupambana na Ugaidi la Shanghai; hatua muhimu ya ushirikiano wa kiusalama nje ya mipaka
Sep 10, 2023 04:26Kufuatia uanachama kamili wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, ujumbe kutoka Iran umeshiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano wa 40 wa Baraza la Muundo wa Kieneo wa Kupambana na Ugaidi la jumuiya hiyo.
-
Rais Raisi: Iran inapinga mabadiliko yoyote katika mipaka ya eneo
Sep 10, 2023 01:05Rais Ebrahim Raisi amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga vikali aina yoyote ya uzushaji mivutano na kubadilishwa mipaka ya kihistoria ya eneo hili na akabainisha kwamba Tehran iko tayari kutoa mchango wa kuzuia kufanywa mabadiliko yoyote katika hali ya jiopolitiki ya eneo.