-
Kerry: Makubaliano ya JCPOA hayahitaji baraka za Marekani
Jun 06, 2017 23:18Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani amesema makubaliano ya nyuklia ya Iran yanaweza kuendelea kusimama imara na kutekelezwa pasina na ushiriki wa Washington.
-
Iran yaendelea kufanya mashauriano kuhusu matukio yaliyojiri katika eneo
Jun 05, 2017 23:43Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Muhammad Javad Zarif, amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mawaziri wa mambo ya nje wa Kuwait, Qatar, Lebanon, Algeria na Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya kuhusiana na matukio yanayoendelea kujiri katika eneo.
-
Iran: Kuzorota hali ya mambo katika nchi za Kiarabu ni natija ya safari ya Trump Saudia
Jun 05, 2017 09:48Mkuu wa Kamati ya Siasa za Nje na Usalama wa Taifa katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu amesema kuwa, kuzorota hali ya mambo katika mataifa ya Kiarabu eneo la Ghuba ya Uajemi, kunatokana na uingiliaji wa Marekani na safari ya rais wa nchi hiyo huko Saudia.
-
Kiongozi Muadhamu: Maadui wanafanya njama ya kupotosha Mapinduzi ya Kiislamu
Jun 04, 2017 11:23Kumbukumbu ya mwaka wa 28 tangu alipoaga dunia mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Imam Khomeini (MA) imefanyika leo kwenye haram ya kiongozi huyo kwa kuhutubiwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ambapo maelfu ya watu kutoka maeneo tofauti ya Iran na wageni wa mataifa ya kigeni walihudhuria kumbukumbu hizo.
-
Iran: Kujiondoa US kwenye Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, hakutauathiri
Jun 04, 2017 02:45Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi yaliyofikiwa mjini Paris, Ufaransa mwaka 2015 haitakuwa na taathira yoyote kwenye mkataba huo.
-
Maiti za raia waliouawa wakitoroka Daesh zatapakaa kwenye barabara za Mosul, Iraq
Jun 04, 2017 02:41Shirika moja la misaada ya kibinadamu limeripoti habari ya genge la kigaidi na kitakfiri la Daesh kuua makumi ya raia katika muda wa saa 48 zilizopita wakijarabu kuukimbia mji wa Mosul nchini Iraq.
-
IAEA yasisitiza kuwa Iran imefungamana na JCPOA
Jun 03, 2017 03:21Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umetoa ripoti na kwa mara nyingine umethibitisha kuwa Iran imeheshimu kikamilifu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Kenya na Iran kuimarisha mahusiano ya pande zote
Jun 01, 2017 23:53Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Kenya, Hadi Farajvand amesema kuwa, mahusiano ya Kenya na Iran hususan katika uga wa uchumi, yamestawi sana katika miaka ya hivi karibuni.
-
Putin akariri umuhimu wa Iran katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria
May 31, 2017 22:49Kwa mara nyingine tena Rais Vladimir Putin wa Russia amesisitiza juu ya umuhimu na nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Syria.
-
Iran yalaani hujuma ya Kabul, idadi ya waliouawa yapindukia 80
May 31, 2017 10:30Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali shambulizi la kigaidi lililoutikisa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul na kuuwa makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi.