-
Wanafunzi wanne wauawa katika ghasia Kongo
Jan 28, 2019 10:43Wanafunzi watatu na afisa wa polisi wameaga dunia kufuatia ghasia zilizotokea kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kukatika huduma ya umeme na maji.
-
Tshisekedi aapishwa kuwa Rais mpya wa Congo DR + Sauti
Jan 24, 2019 12:27Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amepishwa leo kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo akimrithi Rais Joseph Kabila aliyemaliza muda wake. Hatua hiyo inahesabiwa kuwa ya kwanza katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika ya kukabidhiana madaraka kwa njia ya amani na ya kidemokrasia katika kipindi hote cha miaka 59 iliyopita.
-
UN: 13 wauwa kabla ya kuanza mazungumzo ya kusaka amani CAR
Jan 23, 2019 04:18Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa watu 13 wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku chache kabla ya kuanza duru mpya ya mazungumzo ya amani kati ya serikali na makundi ya upinzani.
-
Mshindi wa urais DRC, Tshisekedi, apata uungaji mkono wa AU, EU
Jan 22, 2019 23:19Nchi za Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Ulaya (EU) zimesema zimetilia maanani uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo imetangaza kutambua ushindi wa Felix Tshisekedi katika uchaguzi wa rais nchini humo.
-
Hafla ya kumuapisha rais mpya wa Kongo DR yaakhirishwa
Jan 22, 2019 04:20Sherehe za kumuapisha rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilizotazamiwa kufanyika leo Jumanne zimeakhirishwa na sasa zitafanyika baadaye wiki hii.
-
Mahakama ya DRC yathibitisha kuwa Tshisekedi ndiye mshindi halali wa urais
Jan 20, 2019 04:31Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imemtangaza Felix Tshisekedi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Disemba 30 mwaka uliomalizika.
-
Congo DR yakataa wito wa AU wa kuchelewesha tangazo la matokeo ya mwisho ya uchaguzi mkuu
Jan 18, 2019 12:46Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekataa wito wa Umoja wa Afrika (AU) wa kuchelewesha kutangaza matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa rais, suala ambalo linazidisha shaka kuhusu matokeo ya uchaguzi huo.
-
UN: Watu karibu 900 wameuawa katika mapigano ya kikabila DRC
Jan 17, 2019 04:21Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya 890 wameuawa katika ghasia za kikabila zilizotokea huko kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwezi uliopita wa Disemba 2018.
-
Baraza la Usalama UN lazitaka pande zote Kongo DR ziheshimu matokeo ya uchaguzi
Jan 16, 2019 04:26Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limezitaka pande zote nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ziheshimu matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo.
-
SADC yaitisha kikao cha dharura kujadili mgogoro wa kisiasa Kongo DR
Jan 16, 2019 00:59Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) inatazamiwa kufanya kikao cha dharura kesho Alkhamisi, kujadili mgogoro wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, uliobuka baada ya kutangazwa matokeo tata ya uchaguzi wa urais.