-
UN: Watu milioni moja wamekuwa wakimbizi mkoa wa Kasai, Kongo DR
Apr 21, 2017 23:14Mapigano makali kati ya askari wa serikali ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wanamgambo wa kundi moja la kikabila katika mkoa wa Kasai yamewalazimisha watu zaidi ya milioni moja kuyaacha makazi yao katika kipindi cha miezi minane iliyopita.
-
UN yagundua makuburi mengine 17 ya umati nchini Kongo DR
Apr 19, 2017 10:55Timu ya wachunguzi ya Umoja wa Mataifa imegundua makaburi mengine 17 ya umati katika mkoa wa Kasai, katikati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wiki mbili baada ya makaburi mengine kugunduliwa katika eneo hilo.
-
Zaidi ya raia elfu 9 wa Kongo DR wakimbilia Angola kutafuta hifadhi
Apr 18, 2017 11:07Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia nchi jirani ya Angola kwenda kuomba hifadhi kutokana na kushtadi machafuko nchini mwao.
-
SAUTI: Uteuzi wa Bruno Tshibala kuwa Waziri Mkuu Kongo DR, waufanya uhusiano wa nchi hiyo na Ubelgiji kuingia doa
Apr 14, 2017 12:53Uhusiano kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ubelgiji, umeingia doa kufuatia masuala ya kisiasa yanayoshuhudiwa ndani ya nchi hiyo ya katikati mwa Afrika.
-
Makumi ya waandamanaji watiwa nguvuni Kongo DR
Apr 12, 2017 02:43Makumi ya watu wametiwa mbaroni kwa kushiriki maandamano yaliyopigwa marufuku na serikali katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wapinzani wapigwa marufuku kufanya maandamano Congo DR
Apr 10, 2017 03:07Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano ya kambi ya upinzani.
-
Makaburi mengine 13 ya umati yapatikana katikati ya DRC
Apr 03, 2017 22:59Mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza habari ya kugunduliwa makaburi mengine mengi ya umati katikati ya nchi hiyo.
-
Jeshi la DRC lazima shambulizi la waasi wa Mai-Mai
Apr 02, 2017 09:47Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limefanikiwa kuzima shambulizi la waasi wa Mai-Mai katika kijiji kimoja cha mashariki mwa nchi hiyo na kuwalazimisha waasi hao kukimbia.
-
ICC yatahadharisha kuhusu ukatili unaofanyika Congo DR
Mar 31, 2017 22:52Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imetahadharisha kuwa ukatili uliofanyika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa ni pamoja na mauaji ya wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa unaweza kutambuliwa kuwa ni jinai ya kivita.
-
Machafuko yashtadi Kongo DR, Angola yafunga mpaka wake na nchi hiyo
Mar 31, 2017 10:25Serikali ya Angola imeamua kufunga mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokana na kushtadi machafuko katika mkoa wa Kasai, kusini mwa DRC.