Wapinzani wapigwa marufuku kufanya maandamano Congo DR
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27554-wapinzani_wapigwa_marufuku_kufanya_maandamano_congo_dr
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano ya kambi ya upinzani.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 10, 2017 03:07 UTC
  • Wapinzani wapigwa marufuku kufanya maandamano Congo DR

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku maandamano ya kambi ya upinzani.

Polisi ya Congo imetangaza kuwa, maandamano yaliyoitishwa na wapinzani wa serikali kote nchini hayataruhusiwa. Tangazo hilo limetolewa baada ya kambi ya upinzani kuitisha maandamano ya nchi nzima baada ya Rais Joseph Kabila kumteua Waziri Mkuu mpya ambaye haridhiwi na kambi ya upinzani.

Maandamano hayo yalipangwa kufanyika Jumatatu ya leo mjini Kinshasa na miji mingine ya nchi hiyo. Hata hivyo jeshi la polisi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limetangaza kuwa litatawanya mkusanyiko wowote wenye zaidi ya watu 10.

Chama kikuu cha upinzani cha UDPS katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kimevitaka vyama vyote vya upinzani kushiriki katika maandamano ya leo.

Mamia ya watu wameuawa Congo katika ghasia na machafuko

Mgogoro wa kisiasa katika Congo DR ulianza baada ya Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo kukataa kuondoka madarakani licha ya kipindi chake cha muhula wa pil kumalizika. Ripoti zinasema tangu mwezi Septemba mwaka jana hadi sasa watu 400 wameuawa nchini humo katika ghasia na machafuko yanayoendelea kwenye miji mbalimbal;i ya nchi hiyo.