-
Iran: Itibari ya JCPOA inategemea kuheshimiwa makubaliano hayo na pande zote
Dec 13, 2016 04:39Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kufanikiwa makubaliano ya nyuklia kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi za kundi la 5+1 kunategemea iwapo pande zote zitayaheshimu na kuyatekeleza makubaliano hayo ipasavyo au la.
-
IAEA yathibitisha kuwa Iran imefungamana na JCPOA
Dec 07, 2016 03:52Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA umesema hatua ya Iran kuuza nje ya nchi maji mazito ya nyuklia ni katika sehemu ya kuonyesha kufangamana kwake na makubaliano ya nyuklia.
-
Iran Kuchukua hatua kali kuhusu ukiukwaji wa mapatano ya nyuklia
Dec 06, 2016 02:28Iran itachukua hatua kali na imara iwapo kutakuwepo ukiukwaji wowote wa mapatano ya nyuklia baina yake na madola sita makubwa duniani.
-
Iran yalaani ukatili dhidi ya Waislamu nchini Myanmar
Dec 05, 2016 11:57Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani ubaguzi na ukatili unaofanywa dhidi ya makundi ya kidini nchini Myanmar.
-
Rais Hassan Rouhani: Muswada wa Bunge la Marekani ni ukiukaji wa JCPOA
Dec 04, 2016 11:25Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa la Iran litachukua hatua madhubuti na za kivitendo mkabala na uvunjaji ahadi, kigugumizi na ucheleweshaji wa aina yoyote ile katika kutekeleza mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
-
Waziri Mkuu wa Uingereza aunga mkono makubaliano ya nyuklia Iran
Dec 01, 2016 04:15Msemaji wa Theresa May Waziri Mkuu wa Uingereza amesema kuwa Bi May anaunga mkono kikamilifu Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na anataka kutekelezwa kikamilifu makubaliano hayo.
-
Iran: Tutajibu hatua yoyote ya Marekani ya kuvunja JCPOA
Nov 30, 2016 12:59Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Nje ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, kama Marekani itarefusha vikwazo dhidi ya Iran, basi Jamhuri ya Kiislamu itaongeza kiwango cha urutubishaji wake wa urani kwa "SWU" laki moja na 90 elfu.
-
Onyo la mkuu wa CIA kwa Trump kuhusu JCPOA
Nov 30, 2016 09:42John O. Brennan, Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA amemuonya Donald Trump, rais mteule wa Marekani kutokana na msimamo wake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 yanayojulikana kwa jina la JCPOA na kusisitiza kuwa, haitakuwa busara hata kidogo kufutwa makubaliano yaliyotiwa saini na Tehran na Washington.
-
Kiongozi Muadhamu: Kuendeleza vikwazo dhidi ya Iran ni kinyume na JCPOA
Nov 23, 2016 11:50Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, hatua ya kurefusha vikwazo dhidi ya Iran kwa miaka 10 zaidi, bila ya shaka yoyote ni uvunjaji wa makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kwa jina maarufu la JCPOA.
-
Iran na Ufaransa zasisitiza umuhimu wa kutekelezwa JCPOA
Nov 19, 2016 04:35Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ufaransa zimesisitizia umuhimu wa kutekelezwa makubaliano ya nyuklia ya Vienna, yaliyosainiwa kati ya Iran na nchi za kundi la 5+1.