-
Waisrael washadidisha maandamano ya kumtaka Netanyahu ajiuzulu
Feb 16, 2018 23:11Maelfu ya Waisraeli wamefanya maandamano katika mji mkuu Tel Aviv kushinikiza kujiuzulu Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel, siku chache baada ya polisi ya Israel kupendekeza Benjami Netanyahu afunguliwe mashitaka kutokana na kashfa za ufisadi wa kifedha anazokabiliwa nazo.
-
Wimbi la pili la maandamano ya wananchi nchini Bahrain laanza kwa mnasaba wa Februari 14
Feb 14, 2018 13:19Wimbi la pili la maandamano na harakati ya malalamiko ya wananchi nchini Bahrain kwa mnasaba wa mwaka wa saba wa mapinduzi ya tarehe 14 Februari, limeanza jioni ya leo Jumatano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Watu kadhaa wauawa katika maandamano nchini Guinea
Feb 13, 2018 04:01Kwa akali watu wawili wamethibitishwa kupoteza maisha katika ghasia zilizotokana na maandamano yaliyofanyika jana Jumatatu nchini Guinea Conakry.
-
Warundi waandamana Bujumbura kupinga ripoti ya Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi yao
Feb 11, 2018 01:14Maelfu ya raia wa Burundi Jumamosi ya jana waliandama mjini Bujumbura, katika kulalamikia ripoti ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayopinga suala la kufanyiwa marekebisho katiba ya nchi hiyo ili kumruhusu Rais Pierre Nkurunziza kugombea katika uchaguzi ujao.
-
Malalamiko dhidi ya Trump Sudan Kusini
Feb 07, 2018 08:55Watu wa Sudan Kusini wamefanya maandamano nchini humo wakilalamikia amri mpya ya Rais Doland Trump wa Marekani ya kupiga marufuku jeshi la nchi hiyo ya Kiafrika kuuziwa silaha.
-
Maandamano London ya kupinga kuuziwa silaha Riyadh
Feb 05, 2018 04:23Makumi ya watu juzi waliandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Saudi Arabia mjini London Uingereza wakipinga na kulalamikia hatua ya Uingereza ya kuiuzia silaha Saudia.
-
Wanigeria waendeleza maandamano ya kutaka Sheikh Zakzaki aachiliwe huru.
Feb 04, 2018 04:32Wanachama wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria wanaendeleza maandamano ya amani ya kutaka aachiliwe huru kiongozi wa harakati hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky.
-
Wapalestina wavuruga warsha ya Marekani Ukingo wa Magharibi
Jan 30, 2018 23:52Wapalestina wenye ghadhabu wamevuruga warsha ya biashara iliyoandaliwa na Marekani katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Papa asikitishwa na mauaji ya waandamanaji Kongo DR
Jan 24, 2018 10:39Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ametoa mwito wa kukomeshwa mauaji na ukandamizaji unaofanywa na maafisa usalama dhidi ya waandamanaji katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Maelfu ya watu waandamana kupinga safari ya Trump nchini Uswisi
Jan 24, 2018 04:25Maelfu ya raia wa Uswisi wameandamana mjini Zurich na katika miji mingine muhimu ya nchi hiyo ikiwemo ya Geneva, Lausanne na Fribourg kupinga Rais Donald Trump wa Marekani kuhudhuria kongamano la kila mwaka la Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) linalofanyika katika mji wa Davos.