Malalamiko dhidi ya Trump Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i40037-malalamiko_dhidi_ya_trump_sudan_kusini
Watu wa Sudan Kusini wamefanya maandamano nchini humo wakilalamikia amri mpya ya Rais Doland Trump wa Marekani ya kupiga marufuku jeshi la nchi hiyo ya Kiafrika kuuziwa silaha.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2018 08:55 UTC
  • Malalamiko dhidi ya Trump Sudan Kusini

Watu wa Sudan Kusini wamefanya maandamano nchini humo wakilalamikia amri mpya ya Rais Doland Trump wa Marekani ya kupiga marufuku jeshi la nchi hiyo ya Kiafrika kuuziwa silaha.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press mamia ya Wasudan Kusini jana Jumanne walifanya maandamano mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji kuu wa Sudan Kusini, Juba, ambapo walilalamikia hatua hiyo ya Trump kupiga marufuku uuzwaji silaha za Marekani kwa jeshi la Sudan ksuini.

Wasudan Kusini wanaokimbia mapigano ya ndani

Waandamaaji waliokuwa wamebeba mabango  yaliyosema, 'mauti kwa Trump' na 'Trump usilidhoofishe taifa letu', waliituhumu Marekani kwa kuwaunga mkono waasi wa Sudan Kusini kupitia ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko nchini humo na pia kupitia nchi jirani. Siku ya Ijumaa Marekani ilianza kutekeleza marufuku ya silaha ya upande mmoja dhidi ya Sudan Kusini. Nchi hiyo ya Kiafrika imekuwa ikikabiliwa na vita vya ndani tokea mwaka 2013 ambavyo vimesababisha maafa na migogoro mingi ya kiusalama nchini humo.