-
Mafuriko yaua zaidi ya watu 50 kaskazini mwa Chad
Aug 16, 2024 10:39Watu wasiopungua 54 wamefariki dunia kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika jimbo la Tibesti la kaskazini mwa Chad.
-
Mafuriko kaskazini mwa Sudan yaua na kujeruhi makumi ya watu
Aug 07, 2024 03:20Shirika rasmi la Habari la Sudan (SUNA) limeripoti kuwa watu 11 wamefariki dunia na wengine 60 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha mafuriko katika mji wa Abu Hamad kaskazini mwa Sudan. Mvua hiyo imebomoa makumi ya nyumba huku timu za uokoaji zikiendelea kusaka watu waliotoweka na wengine walionasa chini ya vifusi.
-
Mvua kubwa yazidisha mateso ya wakimbizi mashariki mwa Sudan
Jul 27, 2024 07:02Mvua kubwa inayoendelea kunyesha huko mashariki mwa Sudan imezidisha mateso ya watu waliokimbia makazi yao haswa katika miji ya Gedaref, Kassala na Halfa Aj Jadeedah.
-
Maporomoko ya udongo yaua mamia ya watu New Papua Guinea
May 25, 2024 11:02Mamia ya watu wameripotiwa kuaga dunia kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko Papua New Guinea (PNG).
-
Kiongozi Muadhamu: Kushiriki katika uchaguzi ilikuwa jihadi ya watu wa Iran
Mar 05, 2024 11:25Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameshukuru mahudhurioa ya taifa la Iran katika vituo vya kupigia kura Machi Mosi na kusema: "Kushiriki taifa la Iran katika uchaguzi huo lilikuwa jukumu la kijamii, kiustaarabu na kijihadi."
-
UN: Maelfu wanahitaji msaada wa dharura DRC kutokana na mafuriko
Jan 13, 2024 11:50Umoja wa Mataifa umesema mamia ya maelfu ya watu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanahitaji msaada wa dharura kutokana na athari za mafuriko katika pembe mbali mbali za nchi hiyo.
-
Mvua, maporomoko ya udongo yaua makumi ya watu DRC
Dec 27, 2023 06:43Watu wasiopungua 22 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mji wa Kananga, katikati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
WFP: Karibu watu milioni 3 wameathiriwa na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko Afrika Mashariki
Dec 09, 2023 02:29Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetahadharisha kuhusu tishio linaloongezeka kwa usalama wa chakula Afrika Mashariki kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi za ukanda huo
-
Zoezi la uokoaji laendelea Hanang huku Tanzania ikiomba msaada wa kimataifa kwa wahanga wa maporomoko
Dec 06, 2023 03:39Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameiomba jumuiya za kimataifa na taasisi za ndani kusaidia juhudi za serikali ya nchi hiyo za uokoaji na kutafuta maiti wa maporomoko ya tope pamoja na misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara.
-
Rais Ruto: Kenya imeweka mikakati ya kukabiliana na athari za mafuriko
Nov 25, 2023 13:36Rais William Ruto wa Kenya amesema serikali yake imeweka mipango ya kuwasaidia raia ambao wameathirika na mafuriko yanayoendelea kuripotiwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwenye kanda ya Afrika Mashariki.