-
HRW: Askari usalama Msumbiji wanakiuka haki za binadamu
Dec 05, 2018 01:10Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limevituhumu vyombo vya usalama vya Msumbiji kuwa vinakiuka haki za binadamu katika operesheni zake za kupambana na ugaidi kaskazini mwa nchi.
-
Al Shabab 200 wapandishwa kizimbani nchini Msumbiji
Oct 05, 2018 03:03Maafisa wa mahaka za Msumbiji wametangaza kuwa wamewahukumu wanachama 200 wa kundi la kigaidi la al Shabab.
-
Hujuma za kigaidi zalipuka tena Msumbiji, 12 wauawa
Sep 21, 2018 13:46Kundi la kigaidi linaloaminika kuwa na mfungamano na al-Shabaab ya Somalia limevamia kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na kuua watu 12 na kujeruhiwa wengine kadhaa.
-
Ripoti: Mashambulizi ya 'kigaidi' Msumbiji yameua watu 39 tangu Mei
Jun 20, 2018 07:42Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kwa akali watu 39 wameuawa katika mashambulizi yanayoaminika kuwa ya kigaidi huko kaskazini mwa Msumbiji tangu mwezi Mei mwaka huu hadi sasa.
-
Magaidi wafanya mauaji mengine ya kinyama nchini Msumbiji
Jun 06, 2018 07:27Kundi la kigaidi linaloaminika kuwa na mfungamano na al-Shabaab ya Somalia limevamia kijiji kimoja katika mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na kuua watu saba kwa kuwakata vichwa.
-
Magaidi waua watu 10 kwa kuwakata vichwa nchini Msumbiji
May 29, 2018 13:46Kundi moja la kigaidi limevamia kijiji cha Monjane kaskazini mwa Msumbiji na kuua watu kumi wakiwemo watoto wadogo kwa kuwakata vichwa.
-
Afonso Dhlakama, kiongozi wa zamani wa waasi Msumbiji, afariki dunia
May 04, 2018 13:39Kiongozi wa zamani wa waasi nchini Msumbuji, Afonso Dhlakama, ambaye alikuwa agombee urais mwakani, amefariki dunia Alhamisi akiwa na umri wa miaka 65.
-
Rais wa Msumbiji awapiga kalamu nyekundu mawaziri wanne
Dec 13, 2017 15:18Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amewafuta kazi mawaziri wanne wakiwemo wa mambo ya nje na mafuta. Hata hivyo ofisi yake haijatoa sababu ya kupigwa kalamu nyekundu mawaziri hao.
-
Rais wa Msumbiji awafuta kazi wakuu wa upelelezi na majeshi
Oct 25, 2017 07:08Rais wa Msumbiji amewavuta kazi Mkuu wa Shirika la Upelelezi na Mkuu wa Majeshi ya nchi hiyo wiki mbili baada ya mauaji ya watu 16 katika shambulizi lililofanyika kaskazini mwa nchi hiyo.
-
16 wauawa katika mapigano na polisi nchini Msumbiji
Oct 08, 2017 04:46Watu 16 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi katika mji mmoja mdogo wa kaskazini mwa Msumbiji. Polisi wawili na watu 14 wenye silaha wameuawa katika mlolongo wa mashambulizi dhidi ya vituo vya polisi katika mji mdogo wa Mocimboa de Praia, kaskazini mwa Msumbiji.