Al Shabab 200 wapandishwa kizimbani nchini Msumbiji
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i48582-al_shabab_200_wapandishwa_kizimbani_nchini_msumbiji
Maafisa wa mahaka za Msumbiji wametangaza kuwa wamewahukumu wanachama 200 wa kundi la kigaidi la al Shabab.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 04, 2018 23:33 UTC
  • Al Shabab 200 wapandishwa kizimbani nchini Msumbiji

Maafisa wa mahaka za Msumbiji wametangaza kuwa wamewahukumu wanachama 200 wa kundi la kigaidi la al Shabab.

Maafisa hao wamesema kuwa, mahabusu 200 wanaotuhumia kuwa wanachama wa kundi la kigaidi la al Shabab waliokuwa wakihusika na vitendo vya kigaidi na kuzusha ghasia katika maeno yenye utajiri wa mafuta ya kaskazini mwa nchi hiyo wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Ripoti zinasema kuwa, 50 kati ya watuhumiwa hao ambao walitokea nchi jirani ya Tanzania wamehukumiwa katika gereza ya mkoa wa Cabo Delgado. Vijiji vya mkoa huo ulioko kaskazini mwa Msumbiji vimekuwa vikisumbuliwa na mashambulizi ya umwagaji damu ya wanachama wa kundi la al Shabab tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita wa 2017. 

Ripoti ya serikali ya Msumbiji inasema wapiganaji wa kundi la al Shabab wameua raia 50 wa nchi hiyo, wakachoma moto vijiji kadhaa na kuwalazimisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao. 

Kwa sasa serikali ya Msumbiji imetuma askari na polisi katika maeneo ya mpaka wa nchi hiyo na Tanzania na tayari imewakamata mamia ya washukiwa. 

Mwaka uliopita Bunge la Msumbiji lilipasisha sheria inayozidisha adhabu dhidi ya magaidi.