-
Waziri Mkuu aliyepinduliwa Niger ataka mazungumzo kuhitimisha mapinduzi
Aug 06, 2023 03:28Huku baadhi ya nchi za Afrika Magharibi zikijiandaa kuingia kijeshi nchini Niger 'kurejesha' utawala wa kikatiba, Waziri Mkuu wa nchi hiyo aliyepinduliwa pamoja na serikali ya Rais Mohamed Bazoum wa nchi hiyo ametoa mwito wa kufanyika mazungumzo ili kuhitimisha mzozo huo.
-
Mgogoro wa Mapinduzi ya Kijeshi nchini Niger
Aug 05, 2023 08:23Mgogoro wa kisiasa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Niger umeendelea kutawala habari za eneo la Magharibi mwa Afrika.
-
Ujumbe wa ECOWAS waondoka Niger bila kukutana na kiongozi wa mapinduzi
Aug 04, 2023 12:09Ujumbe wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) umeondoka katika mji mkuu wa Niger, Niamey bila kukutana na kiongozi wa mapinduzi, Jenerali Abdourahmane Tchiani, huku rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Bazoum akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kusaidia kurejesha utawala wa kikatiba.
-
Niger yasimamisha matangazo ya France 24 na RFI
Aug 04, 2023 08:07Serikali ya mpito ya kijeshi ya Niger imetangaza kusitisha nchini humo matangazo na shughuli za redio ya Kifaransa ya RFI na televisheni ya France 24 zinazofadhiliwa na serikali ya Ufaransa.
-
Maelfu waandamana Niger wakitaka kufukuzwa askari wa US, Ufaransa
Aug 04, 2023 02:57Maelfu ya wananchi wa Niger wamefanya maandamano katika mji mkuu Niamey, wakitaka kufukuzwa nchini humo mara moja wanajeshi wa Marekani na Ufaransa.
-
Uingiliaji wa kigeni katika mapinduzi ya Niger
Aug 01, 2023 15:06Baada ya kupita takribani wiki moja tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, mgogoro wa kisiasa umeenea katika nchi hiyo na nchi na taasisi za kieneo na kimataifa zimechukua misimamo tofauti katika uwanja huu.
-
Watawala wapya wa Niger wanaonya juu ya uingiliaji wowote wa kijeshi wa kigeni, Ulaya yatishia kuwawekea vikwazo
Jul 29, 2023 03:37Watawala wapya wa kijeshi nchini Niger wameonya dhidi ya uingiliaji wowote wa majeshi ya kigeni nchini humo baada ya kumtangaza Jenerali Abdourahmane Tchiani, Mkuu wa Gadi ya Rais wa Niger, kuwa kiongozi wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika; huku Umoja wa Ulaya na Ufaransa zikitishia kuiwekea Niger vikwazo.
-
Jenerali Tchiani atangazwa mkuu wa serikali ya mpito Niger
Jul 28, 2023 12:15Jenerali Abdourahmane Tchiani, Mkuu wa Gadi ya Rais wa Niger ameteuliwa kuwa kiongozi wa serikali ya mpito ya nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika, siku moja baada ya jeshi la nchi hiyo kutangaza kuwa limemuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum.
-
UN yalaani mapinduzi ya kijeshi Niger; wananchi waandamana
Jul 27, 2023 10:53Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa akilaani vikali mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum wa Niger.
-
Magaidi 55 waangamizwa katika operesheni ya pamoja ya majeshi ya Niger na Nigeria
May 30, 2023 06:15Jeshi la Niger limetangaza kuwa wanajeshi wawili na magaidi 55 wakiwemo makamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi la DAESH(ISIS) Afrika Magharibi wameuawa katika operesheni ya pamoja iliyotekelezwa na jeshi hilo na lile la Nigeria.