-
Oman yataka Israel ibebeshwe dhima kwa jinai zake huko Gaza
Nov 01, 2023 03:02Oman imeitaka jamii ya kimataifa iibebeshe dhima Israel kwa jinai zake za kutisha katika Ukanda wa Gaza, na pia dunia ichukue hatua za dharura za kukomesha mauaji ya halaiki ya Wapalestina wasio na hatia.
-
Alkhamisi tarehe 28 Septemba, 2023
Sep 28, 2023 03:03Leo ni Alkhamisi tarehe 12 Mfunguo Sita Rabiul Awwal 1445 Hijria sawa na Septemba 28, 2023.
-
Baqeri: Ghuba ya Uajemi inahitaji usalama wa nchi za eneo tu
Sep 22, 2023 02:44Mkuu wa Komandi Kuu ya Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa uwepo wa kijeshi wa maajinabi katika Ghuba ya Uajemi na kusisitiza kuwa, nchi za eneo hili zina uwezo wa kujidhaminia usalama wao.
-
Viongozi wa Iran na Oman watilia mkazo kupanuliwa mashirikiano baina ya nchi mbili
Aug 01, 2023 13:36Viongozi wa Iran na Oman wamesisitiza na kutilia mkazo nia ziliyonayo Tehran na Muscat ya kuinua kwa kiwango na upeo wa juu zaidi uhusiano wa nchi mbili na kupanua zaidi maelewano baina ya pande mbili.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran inakaribisha kuhuishwa uhusiano wake na Misri
May 29, 2023 11:32Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Iran inakaribisha azma ya kufufuliwa uhusiano wake na Misri.
-
Sultani Haitham wa Oman awasili nchini na kulakiwa rasmi na Rais Raisi
May 28, 2023 14:27Hafla rasmi ya kumkaribisha Sultani Haitham Bin Tariq Al Saeed wa Oman, ambaye ametembelea Iran kwa mara ya kwanza akiwa Mfalme wa Oman, imefanyika katika jumba la kiutamaduni na kihistoria la Saad Abad hapa mjini Tehran.
-
Mufti wa Oman aunga mkono majibu ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina
May 12, 2023 05:44Mufti Mkuu wa Oman amesema kuwa, majibu ya kishujaa ya wanamapambano wa Palestina ya kupiga kwa makombora maeneo ya Wazayuni ni majibu ya jinai za Israel dhidi ya taifa linalodhulumiwa la Palestina na amewataka Waislamu kuwa pamoja na taifa hilo linalodhulumiwa kwani mapanmbano yao yanauwakilishi umma mzima wa Kiislamu.
-
Mufti wa Oman asisitiza udharura wa kuungwa mkono Wapalestina ili kuzuia hujuma za Wazayuni
Apr 07, 2023 02:21Mufti wa Oman ametoa amepinga vikali hujuma zinazoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina katika Msikiti Mtukufu wa al Aqsa na ametaoa wito wa kuungwa mkono Palestina.
-
Hussein Amir-Abdolllahian: Oman ni jirani na rafiki wa kuaminika wa Iran
Mar 31, 2023 11:37Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Oman ni jirani na rafiki wa kuaminika wa Iran na kwamba, mashirikiano baina ya mataifa haya mawili yataongezeka na kuimarika zaidi.
-
Iran na Oman zajadili kuondolewa vikwazo Tehran
Mar 25, 2023 07:23Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian amezungumza na mwenzake wa Oman, Badr Albusaidi kwa njia ya simu, na wawili hao wamejadili kuhusu hali ya sasa ya mazungumzo ya kuiondolea Jamhuri ya Kiislamu vikwazo vya kidhalimu.