-
Waingereza waandamana kuonyesha mshikamano wao na Wapalestina
Apr 01, 2018 12:51Wananchi na makundi ya kiraia katika mji wa London nchini Uingereza wamefanya maandamano wakitangaza uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina na kulaani jinai wanazofanyiwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
SEPAH: Tutafanya juu chini kuwasaidia Wapalestina
Apr 01, 2018 03:14Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH sanjari na kulaani mauaji ya Wapalestina 17 waliokuwa wakiandamana kwa amani Ijumaa ya juzi katika mpaka wa Gaza ili kuadhimisha Siku ya Ardhi, limesema litafanya kila liwezekanalo kuwasaidia Wapalestina wapate haki zao.
-
Netanyahu awashukuru askari katili wa Israel waliowaua Wapalestina Ghaza
Apr 01, 2018 03:06Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amewapongeza na kuwashukuru wanajeshi wa utawala huo haramu waliowaua na kuwajweruhiwa mamia ya Wapalestina waliokuwa wakifanya maandamano ya amani hivi karibuni katika mpaka wa Ghaza, kushinikiza kurejea katika ardhi zao zilizoghusubiwa.
-
Israel imetegemea fatuwa za Mashekhe wa Saudia kuwaua Wapalestina
Mar 31, 2018 11:37Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel linasema linawaua Wapalestina wanaoandamana kwa kutegemea fatuwa ya mashekhe wa Kiwahhabi kutoka Saudi Arabia.
-
Iran yalaani utawala wa Kizayuni kwa kuwaua Wapalestina katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza
Mar 31, 2018 11:20Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mauaji ya Wapalestina wasiopungua 17 ambao walikufa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala wa kibaguzi wa Israel katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza.
-
Hizbullah: Matukio ya Ghaza yamethibitisha kwamba matukufu ya Palestina bado yanaenziwa
Mar 31, 2018 03:17Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon imetoa taarifa kufuatia maandamano makubwa ya Ijumaa ya jana mjini Ghaza Palestina na kusema kuwa, matukio hayo yamethibitisha kwamba matukufu ya Palestina bado yanaendelea kuenziwa na kwamba Wapalestina wako tayari kujitolea kila kitu chao katika njia ya ukombozi wa ardhi zao.
-
Wapalestina 8 wauawa shahidi na jeshi la Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi
Mar 30, 2018 11:24Kwa akali Wapalestina wanane wameuawa shahidi na wanajeshi katili wa Israel katika maandamano ya Siku ya Ardhi, ya kulaani hatua ya utawala huo ghasibu ya kupora ardhi zao, yaliyofanyika leo karibu na uzio wa kibaguzi wa Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
UNRWA: Wapalestina Ghaza wanakabiliwa na hali mbaya kibinadamu
Mar 29, 2018 02:06Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi wa Palestina Bw. Pierre Krahenbuhl ameonya kuhusu kuendelea kuwa mbaya hali ya kibinadamu ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Gaza ambalo liko chini ya mzingiro wa Utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Oman yahimiza kuungwa mkono haki za wananchi wa Palestina
Mar 28, 2018 11:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameyahimiza mataifa ya dunia kuunga mkono haki za wananchi wa Palestina na mapambano yao hadi watakapopata ushindi na uhuru wao.
-
HAMAS: Vitisho vya Israel haviwezi kuzuia kufanyika maandamano ya haki ya kurejea makwao Wapalestina
Mar 28, 2018 02:43Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, vitisho vya utawala dhalimu wa Israel katu haviwezi kuzuia kufanyika maandamano makubwa ya haki ya kurejea makwao Wapalestina.