-
Kan'ani Chafi: Mashambulio mapya dhidi ya Gaza ni kashfa kubwa ya kimaadili kwa Marekani
Dec 02, 2023 23:45Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ameandika katika kujibu idhini ya Marekani kwa mashambulizi mapya yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza kwamba, hii ni kashfa kubwa ya kimaadili kwa serikali ya Marekani na imeonyesha sura halisi ya haki za binadamu ya Washington kwa walimwengu.
-
Nukta nne za kistratijia katika matamshi ya Kiongozi Muadhamu kuhusu Asia Magharibi na kadhia ya Palestina.
Dec 02, 2023 00:50Akizungumza siku ya Jumatano tarehe 29 Novemba katika kikao na askari wa kujitolea mashuhuri kama Basij kutoka pembe zote za nchi, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, amegusia nukta kadhaa muhimu kuhusu operesheni ya Kimbunga cha al-Aqsa na stratijia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusiana na kadhia ya Palestina.
-
Israel yaanza tena kumwaga damu za Wapalestina Gaza, makumi wauawa shahidi
Dec 01, 2023 04:25Miripuko kadhaa na milio ya risasi imesikika kaskazini mwa Ukanda wa Gaza baada ya utawala haramu wa Israel kuanzisha tena hujuma na mashambulizi yake ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu, baada ya muda wa usitishaji vita kumalizika mapema leo.
-
Waziri Mkuu wa Uhispania: Israel haiheshimu sheria za kimataifa za ubinadamu
Dec 01, 2023 03:16Waziri Mkuu wa Uhispania amesema kwamba, kwa kuzingatia idadi ya raia wakiwemo watoto wadogo ambao ni wahanga wa vita vya wiki kadhaa vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza, ni wazi kuwa Tel Aviv haiheshimu sheria za kimataifa za ubinadamu.
-
Iran yaipongeza Yemen kwa kuwaunga mkono Wapalestina
Nov 30, 2023 23:51Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amepongeza na kusifu uungaji mkono wa Yemen kwa taifa la Palestina, wakati huu ambapo utawala wa Kizayuni umeshadidisha jinai zake dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
-
Washington Post: Chama tawala India kinatumia vita vya Israel dhidi ya Gaza kuwadhihirisha Waislamu kuwa ni mashetani
Nov 30, 2023 22:59Gazeti la Washington Post la Marekani limetahadharisha kuhusu mienendo ya chama tawala nchini India na jinsi kinavyotumia vibaya vita vya Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza na kuwadhihirisha Waislamu kuwa ni 'mashetani'.
-
Israel yaendelea kumwaga damu za watoto wadogo Jenin
Nov 30, 2023 00:24Watoto wawili wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Jenin, kaskazini ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Iran: Wapalestina wataamua hatima yao wenyewe
Nov 27, 2023 07:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema taifa la Palestina halitaruhusu ama utawala wa Kizayuni au Marekani kufikia malengo yao haramu, na kusisitiza kuwa hatima ya Palestina ipo mikononi mwa Wapalestina wenyewe.
-
Jihad Islami: Israel imeshindwa kuusambaratisha muqawama
Nov 27, 2023 07:14Mjumbe wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema utawala wa Kizayuni wa Israel haujafikia hata moja ya malengo yake ya kuanzisha mashambulizi ya kinyama dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza, hasa azma ya utawala huo ya kuusambaratisha mrengo wa muqawama.
-
Israel yaua shahidi Wapalestina 4 Jenin, Ukingo wa Magharibi
Nov 25, 2023 23:47Vijana wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Jenin, kaskazini ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.