Israel yaua shahidi Wapalestina 4 Jenin, Ukingo wa Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i105250-israel_yaua_shahidi_wapalestina_4_jenin_ukingo_wa_magharibi
Vijana wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Jenin, kaskazini ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Nov 25, 2023 23:47 UTC
  • Israel yaua shahidi Wapalestina 4 Jenin, Ukingo wa Magharibi

Vijana wanne wa Kipalestina wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Jenin, kaskazini ya eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Shirika la habari la Palestina la Wafa limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wanajeshi wa Kizayuni wamefanya mauaji hayo leo Jumapili, sambamba na kuzingira hospitali za Shahidi Khalil Suleiman na Ibn Sina katika eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu.

Wafa imemnukuu Mkurugenzi wa Hospitali ya Al-Razi akiwatambua wahanga wa jinai hizo za Israel Ukingo wa Magharibi kuwa Ammar Muhammad Abu al-Wafa (21), Ahmed Abu al-Hija (20), Muhammad Mahmoud Fraihat (27) na Mahmoud Khaled Abu al-Hija (17).

Katika hatua nyingine, Idara ya Wafungwa wa Palestina imethibitisha habari ya jeshi la Kizayuni kuwaachia huru wafungwa wengine 39 wa Kipalestina mkabala wa kuachiwa mateka 17 wa Gaza (Waisraeli 13 na raia 4 wa Thailand).

Kabla ya hapo, jeshi la Kizayuni liliwaachia huru wafungwa wengine, ambao ni wanawake 24 na watoto 15, kama sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Kuendelea kuachiwa huru Wapalestina, matunda ya Kimbunga cha al-Aqsa

Usitishaji vita wa siku nne kati ya utawala wa Kizayuni na Harakati ya Muqawama ya Palestina Hamas ulianza kutekelezwa juzi Ijumaa asubuhi, baada ya Wazayuni kuwaua shahidi Wapalestina zaidi ya 15,000.

Utawala huo umekubali kushindwa katika operesheni yake ya kuwakomboa mateka na kusalimu amri mbele ya matakwa ya Wapalestina.

Wanamuqawama wa Palestina walianzisha Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa dhidi ya utawala ghasibu wa Israel mnamo Oktoba 7, ikiwa ni katika kukabiliana na zaidi ya miongo saba ya uvamizi  wa utawala huo dhidi ya watu wa Gaza na maeneo mengine ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.