-
Riek Machar akubali kusaini makubaliano ya mwisho ya amani ya Sudan Kusini
Aug 29, 2018 03:17Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini amekubali kutia saini makubaliano ya mwisho ya mkataba wa amani na serikali ya Juba ambayo yatamaliza mgogoro wa muda mrefu wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
Riek Machar akataa kusaini rasimu ya makubaliano ya amani Sudan Kusini
Aug 28, 2018 07:46Kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini, amekataa kutia sahihi rasimu ya hivi karibuni ya mkataba wa amani na serikali ya Juba ambayo ingemaliza mgogoro wa miaka mingi wa nchi hiyo.
-
Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini kuanza tena mjini Khartoum
Aug 24, 2018 09:04Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yanatarajiwa kuanza tena mjini Khartoum katika nchi jirani ya Sudan Jumatatu ijayo. Mazungumzo hayo yalikuwa yameahirishwa kutokana na sherehe za Idul Adh'ha zilizoanza Jumanne iliyopita.
-
Mahasimu Sudan Kusini wasisitiza kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani
Aug 22, 2018 03:14Pande mbalimbali zinazojihusisha na mchakato wa amani wa Sudan Kusini, zimewasisitizia watu wa nchi hiyo kutekeleza kikamilifu makubaliano ya amani ya Khartoum.
-
UN kuchunguza mauaji ya watu 14 eneo la Kuda Sudan Kusini
Aug 18, 2018 03:00Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umeanza kuchunguza mauaji ya watu 14 waliouawa wakati wa mapigano baina ya jamii za wafugaji nje ya Juba, mji mkuu wa nchi hiyo.
-
Watu 75 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila Sudan Kusini
Aug 14, 2018 10:31Maafisa wa serikali ya Sudan Kusini wametangaza kuwa watu 23 wameuliwa na wengine 52 wamejeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea magharibi mwa nchi hiyo.
-
Rais wa Sudan Kusini awapa msamaha Machar na waasi wengine
Aug 09, 2018 10:47Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ametoa msamaha kwa waasi waliohusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo akiwemo makamu wake wa zamani, Riek Machar.
-
Watoto zaidi ya 100 Sudan Kusini waachiliwa huru na waasi kufuatia jitihada za UNICEF
Aug 07, 2018 10:02Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema askari watoto 128 wameachiwa huru kutoka makundi ya waasi yaliyovunjwa huko Yambio, mkoa wa Western Equatoria kusini mwa Sudan Kusini.
-
Sudan Kusini wasisitiza kuheshimiwa makubaliano ya mwisho wa kugawana madaraka
Aug 06, 2018 03:36Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na hasimu wake mkubwa, Riek Machar wamehimiza kuheshimiwa kikamilifu mapatano ya mwisho ya kugawana madaraka kwa shabaha ya kukomesha vita vya ndani vya umwagaji mkubwa wa damu vilivyodumu kwa miaka mitano sasa.
-
Kiir: Makubaliano mapya ya amani hayatasambaratika
Aug 03, 2018 20:57Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema anaamini kuwa makubaliano mapya ya amani baina ya serikali yake na kundi kubwa zaidi la waasi nchini humo hayatasambaratika kwa sababu sio ya kutwishwa kama yale ya kabla yake.