-
Wasomi Tanzania: Iundwe tume huru ili kuepusha utata wa tuhuma kati ya Tundu Lissu na serikali
Feb 14, 2019 12:12Wasomi na wanasheria nchini Tanzania wametoa mwito wa kuundwa tume huru isiyo na mahusiano na serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa shambulio lililompata Tundu Lissu, Mbunge wa upinzani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hapo Septemba 7 mwaka 2017 na kumaliza utata uliopo kuhusiana na sakata hilo.
-
Sheikh Ponda: Inasikitisha mno Chuo Kikuu cha Dodoma, Tanzania kusitisha ujenzi wa msikiti
Feb 10, 2019 13:41Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda amesema kuwa, jumuiya hiyo imesikitishwa mno na hatua ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kusitisha ujenzi wa msikiti uliokuwa ujengwe chuoni hapo.
-
Balozi Farhang: Miradi ya nyuklia ya Iran ni ya amani kikamilifu + Sauti
Feb 07, 2019 14:26Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, Bw. Mousah Farhang amesema kuwa miradi ya nyuklia ya Iran ni ya amani kikamilifu, kinyume kabisa na propaganda zinazoenezwa na madola ya kibeberu. Ammari Dachi na taarifa kamili kutoka Dar es Salaam...
-
Kesi ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu Tanzania yaanza kusikilizwa
Feb 07, 2019 11:17Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam nchini Tanzania imeanza kusikiliza kesi ya kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi uliofanywa na Rais John Magufuli tarehe Mosi Februari mwaka jana 2018.
-
Mgogoro wa Burundi umeshindikana? Mkapa alia na EAC kumtelekeza
Feb 07, 2019 11:13Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa kuna kila dalili za kuonesha kuwa mgogoro wa Burundi umeshindikana kutatuliwa.
-
Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania azindua mahakama inayotembea
Feb 06, 2019 09:12Rais John Magufuli wa Tanzania amezindua gari maalumu la mahakama inayotembea litakalosaidia kusikiliza kesi katika mikoa ya Mwanza na Dar es Salaam.
-
Taharuki yaibuka mkoani Njombe, Tanzania kutokana na vitendo vya utekaji nyara na mauaji dhidi ya watoto wadogo
Feb 04, 2019 10:46Hali ya taharuki imeendelea kushuhudiwa mkoani Njombe, Tanzania kutokana na vitendo vya utekaji nyara na mauaji dhidi ya watoto wadogo. Vitendo hivyo vimeendelea kushuhudiwa huku serikali ya Tanzania sambamba na kufanya juhudi kubwa zenye lengo la kuzuia jinai hizo, ikitakiwa pia kutoa kauli rasmi itakayoleta utulivu katika eneo hilo.
-
Wazazi Njombe Tanzania walazimika kuacha kazi na kusindikiza watoto shuleni wasiuawe + Sauti
Feb 03, 2019 14:33Wazazi mkoani Njombe nchini Tanzania wameongeza uangalifu kwa watoto wao na wengine wanaacha shughuli zao ili kusindikiza watoto wao shuleni. Hii ni kutokana na wimbi la mauaji ya watoto hao mkoani humo. Amari Dachi na maelezo zaidi kutoka Dar es Salaam...
-
Mkutano wa wakuu wa EAC hatimaye wafanyika Arusha, Tanzania
Feb 01, 2019 10:24Marais wanne kati ya sita wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC, wamewasili Arusha Tanzania, kushiriki mkutano wa wakuu wa jumuiya hiyo ya kikanda ambao mwaka jana ulifutwa mara mbili ndani ya muda wa wiki tatu.
-
Tanzania kuchunguza uchinjaji wa watoto 10 Njombe
Jan 29, 2019 10:25Serikali ya Tanzania imesema itachunguza tukio la kusikitisha la watoto 10 kupoteza maisha baada ya kuchinjwa katika eneo la Njombe.