-
Grossi atahadharisha kuhusu usalama wa kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia
Mar 30, 2023 07:59Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ametoa tahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea maafa katika kituo cha nyuklia cha Zaporizhzhia iwapo kitashambuliwa. Rafael Grossi ametoa indhari hiyo baada ya kukitembelea kituo hicho cha nguvu za nyuklia nchini Ukraine.
-
Amnesty: Vita vya Russia na Ukraine vimeanika undumakuwili uliopo katika haki za binadamu
Mar 28, 2023 06:12Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeeleza katika ripoti yake mpya kuwa kuvamiwa Ukraine na Russia kumeanika undumilakuwili na unafiki uliopo kuhusu haki za binadamu katika uga wa kimataifa, kutokana na jinsi Magharibi ilivyochukua msimamo mkali dhidi ya Russia na kuonyesha "kimya cha uziwi" kwa ukiukaji wa haki za binadamu unaofanyika katika pembe zingine za dunia.
-
Onyo la Russia kuhusu kuzuka vita vya nyuklia kufuatia ongezeko la kutumwa silaha za Magharibi nchini Ukraine
Mar 24, 2023 22:48Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama wa Kitaifa la Russia, ameonya juu ya uwezekano wa kutokea vita vya nyuklia, akisema kuendelea kutumwa silaha nchini Ukraine kunaongeza maradufu uwezekano wa kuibuka hivi karibuni vita vya nyuklia karibu katika eneo.
-
Juhudi za China za kumaliza mgogoro wa Ukraine
Mar 21, 2023 03:22Rais Xi Jinping wa China, amesema kuwa mpango wa nchi yake wa kutatua mzozo wa Ukraine unaakisi maoni ya ulimwengu, na kuwa vipengee 12 vya mpango huo vitaondoa kabisa taathira hasi za mgogoro huo.
-
Undumakuwili wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kuhusu jinai za kivita
Mar 19, 2023 04:11Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ambayo inajiona kuwa mahakama ya kwanza ya kudumu ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa mauaji ya halaiki, jinai dhidi ya binadamu, jinai za kivita na uchokozi, Ijumaa iliyopita ilitoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa Rais Vladmir Putin wa Russia.
-
Vassily Nebenzia: Tutafungua mahakama ya kimataifa ya uhalifu kuhusu Ukraine
Mar 18, 2023 10:50Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa ametoa matamshi yake kuhusu uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu dhidi ya Rais na Kamishna wa Haki za Watoto wa Russia akisema Moscow inajiandaa kufungua kesi kuhusiana na Ukraine.
-
Russia: Malengo yetu Ukraine yataweza kufikiwa kwa operesheni za kijeshi tu
Mar 15, 2023 00:35Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema malengo ya nchi hiyo nchini Ukraine yanaweza kufikiwa kupitia operesheni za kijeshi tu.
-
Russia: Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita nchini Ukraine
Mar 07, 2023 22:54Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema, Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
-
Rais wa Baraza la Usalama UN akwepa kujibu suali kuhusu Palestina na Ukraine
Mar 03, 2023 04:14Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amekataa kujibu suali aliloulizwa kuhusu Palestina na Ukraine.
-
Maandamano dhidi ya vita katika nchi za Ulaya
Feb 27, 2023 08:14Sambamba na kuendelea vita nchini Ukraine na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii katika nchi mbalimbali za Ulaya, wananchi barani humo wamefanya maandamano katika nchi kadhaa wakipinga sera za nchi za Magharibi na kuingilia kati vita vya Ukraine.