Russia: Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita nchini Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i94846-russia_marekani_ndiyo_sababu_kuu_ya_kurefuka_vita_nchini_ukraine
Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema, Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 08, 2023 02:24 UTC
  • Russia: Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita nchini Ukraine

Msemaji wa ofisi ya rais wa Russia amesema, Marekani ndiyo sababu kuu ya kurefuka vita vinavyoendelea nchini Ukraine.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dmitry Peskov amesema, Marekani haitaki vita vya Ukraine viishe na itafanya lolote kuendeleza vita hivyo.
Vita nchini Ukraine pamoja na athari zake zote za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kiutamaduni viko katika mwezi wake wa 13, na nchi za Magharibi bado zinatuma silaha kwa nchi hiyo.
Maafisa wa Russia na baadhi ya wataalamu na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi wamevitaja vita vya Ukraine kuwa ni vita vya niaba na uwakilishi kati ya Magharibi na Russia.
Dmitry Peskov

Moscow imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kuwa kupelekwa silaha za nchi za Magharibi kwa Ukraine kutarefusha tu mzozo katika nchi hiyo na kuwa na matokeo yasiyotabirika.

Nchi za Ulaya na Magharibi, hasa Marekani zimeshadidisha vikwazo dhidi ya Shirikisho la Russia na kwa hatua yao ya kuipatia Kyiv kila aina ya silaha nyepesi na nzito, sio tu hazijachukua hatua yoyote ya kukomesha vita vya Ukraine, lakini pia zimechochea na kukoleza moto wa vita na mapigano katika nchi hiyo.../