-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Imarati, Uturuki wajadiliana matukio ya Ghaza
Apr 11, 2024 06:24Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika mazungumzo yake ya simu na mawaziri wenzake wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) na Uturuki kwamba kuna udharura wa kukomeshwa haraka jinai za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza.
-
Rais Raisi: Kukata uhusiano wa kiuchumi na kisiasa ndiyo silaha bora ya kuipigisha magoti Israel
Apr 10, 2024 23:09Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kukatwa uhusiano wa kiuchumi na kisiasa wa nchi za Waislamu na utawala wa Kizayuni ndiyo silaha bora ya kukomesha jinai za Wazayuni huko Palestina.
-
Wananchi wa Uturuki washiriki katika uchaguzi muhimu wa serikali za mitaa
Mar 31, 2024 07:41Vituo vya kupigia kura nchini Uturuki vilifunguliwa mapema leo asubuhi kuruhusu wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotajwa kuwa ni mtihani muhimu kwa Rais Recep Tayyip Erdogan wa nchi hiyo. Weledi wa mambo wanasema kuwa Rais wa Uturuki anakabiliwa na kibarua kigumu ili kuyarejesha maeneo muhimu ya mijini aliyoshindwa na upinzani miaka mitano iliyopita.
-
Erdogan: Dunia iishinikize Israel itekeleze azimio la Baraza la Usalama la UN
Mar 28, 2024 23:08Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameitaka jamii ya kimataifa iendelee kuushinikiza utawala wa Kizayuni wa Israel utekeleze azimio la kutaka kusitishwa mara moja mapigano huko Gaza, lililopasishwa majuzi na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Kukamatwa mtandao wa kijasusi wa Mossad nchini Uturuki
Jan 05, 2024 23:28Ikiwa ni katika juhudi zinazoendelea za kufuatilia, kufichua na kuvunjwa mitandao ya kijasusi ya Israel nchini Uturuki, serikali ya Ankara kwa mara nyingine imetangaza kuwa mtandao wa kijasusi wa Mossad umegunduliwa nchini humo na baadhi ya wanachama wake kukamatwa.
-
Maandamano ya wananchi wa Uturuki ya kupinga vita
Jan 03, 2024 03:59Katika muendelezo wa maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari ya Waislamu huko Gaza, makumi ya maelfu ya wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa mjini Istanbul kupinga jinai za utawala wa Kizayuni na mauaji ya vijana wa Kituruki kaskazini mwa Iraq katika siku ya kwanza ya mwaka huu mpya wa 2024.
-
Waandamanaji Uturuki: Marekani ndiye shetani halisi
Jan 01, 2024 08:25Kwa mara nyingine tena, wananchi wa Uturuki wamekusanyika nje ya Ubalozi Mdogo wa Marekani mjini Istanbul katika maandamano ya kuonyesha himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza wanaoendelea kukabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel.
-
Rais Erdogan wa Uturuki: Hakuna tofauti kati ya Hitler na Netanyahu
Dec 28, 2023 03:15Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema, "hakuna tofauti" kati ya kile waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu anakifanya katika mashambulizi ya miezi kadhaa sasa huko Gaza na kile kiongozi wa Nazi Adolf Hitler alikifanya miongo kadhaa iliyopita.
-
Msimamo imara wa wananchi na vyama vya Uturuki kuhusu uhusiano na Israeli na uwepo wa Marekani huko Incirlik
Dec 11, 2023 07:30Kufuatia kuendelea jinai za utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Gaza na uungaji mkono mkubwa wa Marekani kwa jinai hizo, wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano mjini Istanbul na kutoa matakwa mapya kwa serikali ya Rais Recep Tayyip Erdogan.
-
Kulaaniwa kimataifa veto ya Marekani dhidi ya azimio la Baraza la Usalama la kusitisha vita vya Gaza
Dec 10, 2023 23:18Kitendo cha kinyama na cha kijinai cha Marekani cha kulipigia kura ya veto azimio la kusitisha vita Gaza katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimeendelea kulaaniwa kimataifa.