-
Chama cha DA cha Afrika Kusini chajiondoa kwenye mazungumzo ya kitaifa
Jun 28, 2025 23:14Chama cha Democratic Alliance cha nchini Afrika Kusini kimejiondoa kwenye mazungumzo ya kitaifa hata hivyo hakijajitoa katika serikali ya mseto baada ya Rais wanchi hiyo Cyril Ramaphosa kumfuta kazi Naibu Waziri wake mmoja. Haya yameelezwa na kiongozi wa chama hicho John Steenhuisen.
-
EACC: Wanafunzi Kenya wanatumiwa na viongozi kusajili kampuni hewa za kupora pesa
Jun 28, 2025 04:58Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi ya Kenya (EACC) imefichua mpango, ambapo maafisa wa juu wa serikali za Kaunti, wakiwemo magavana wanadaiwa kuwahusisha wanafunzi walioko kwenye mafunzo ya kazi kama njia ya kufuja mabilioni ya pesa za umma kupitia kampuni hewa.
-
Amnesty Kenya: Vifo 16 vimesajiliwa kufuatia ghasia zilizojiri nchini
Jun 26, 2025 12:20Watu 16 wameuawa na mamia wamejeruhiwa wakati wa maandamano ya kitaifa dhidi ya serikali nchini Kenya siku ya Jumatano, ambapo kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Amnest Kenya na Kamisheni ya Taifa ya Kenya ya Haki za Binadamu, wengi wao wameuawa na polisi.
-
Jeshi la Sudan linasema limedhibiti tena maeneo muhimu katika jimbo la Blue Nile kutoka kwa RSF
Jun 26, 2025 12:06Jeshi la Sudan limeyadhibiti tena maeneo kadhaa katika jimbo la Blue Nile, kusini mashariki mwa nchi hiyo, yaliyokuwa yakishikiliwa na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) baada ya mapambano ya jeshi la Sudan dhidi ya RSF na wapiganaji wa harakati ya SPLM-N.
-
Waislamu wa Nigeria washerehekea ushindi wa Iran dhidi ya Marekani na Israel
Jun 25, 2025 05:27Waislamu nchini Nigeria wamesherehekea ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya Marekani na utawala haramu wa Israel baada ya vita kati ya Iran na Isreal kusitishwa baada ya kudumu kwa siku 12.
-
Zakzaky: Mashambulizi ya kigaidi ya Israel yanapasa kulaaniwa duniani kote
Jun 16, 2025 03:38Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria (IMN), Sheikh Ibrahim Zakzaky amelaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran na kuelezea hujuma hizo za utawala wa Kizayuni dhidi ya nchi huru kuwa ni kitendo cha juu zaidi cha uchokozi, kinachopaswa kulaaniwa duniani kote.
-
MSF: Unyanyasaji wa kijinsia umeongezeka mashariki mwa DRC
Jun 15, 2025 09:03Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia vimeongezeka mno katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Sheikh Dalhu Abdul Mumin: Mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran ni kitendo cha ugaidi
Jun 15, 2025 08:06Imamu wa Waislamu wa Kishia wa eneo la Kaskazini mwa Ghana, Sheikh Dalhu Abdul Mumin amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Iran na kuyataja kuwa ni "kitendo cha wazi cha kigaidi cha Israel ya Kizayuni dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."
-
Nigeria yalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran
Jun 15, 2025 01:06Nigeria imelaani vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran na kusema uhasama huo wa Israel utatumbukiza eneo la Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) katika hali ya taharuki.
-
Afrika Kusini yalaani mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Iran
Jun 14, 2025 07:20Afrika Kusini usiku wa kumkia leo Jumamosi imelaani mashambulizi ya kigaidi ya Israel dhidi ya Iran na kuhimiza kufanyika juhudi za kidiplomasia za kupunguza mivutano katika eneo la Asia Magharibi.