-
Takriban Wasudan 75,000 wamekimbia Ethiopia kutafuta usalama wao
Jun 14, 2025 07:16Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limetangaza kuwa, takriban Wasudan 75,000 wamekimbia Ethiopia kutafuta usalama wao tangu mgogoro wa uchu wa madaraka baina ya majenerali ulipozuka nchini humo zaidi ya miwili iliyopita.
-
Waliokufa maji katika ajali za boti 2 DRC wapindukia 50
Jun 14, 2025 03:33Watu wasiopungua 52 wamethibitishwa kufariki dunia huku wengine kadhaa wakitoweka baada ya boti mbili za abiria kuzama kwenye maji ya Ziwa Tumba, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Karibu watu 50 waaga dunia kwa mafuriko nchini Afrika Kusini
Jun 12, 2025 08:56Watu karibu 50 wakiwemo wanafunzi wa Shule, wamepoteza maisha Nchini Afrika Kusini kutokana na mafuriko makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kwenye mkoa wa Cape Mashariki.
-
Rais Traore: Mabeberu wanajaribu kuvunja Muungano wa Sahel
Jun 12, 2025 04:22Rais wa mpito wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traoré, amezishutumu nchi za kigeni kwa kujaribu kuhujumu Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES) kwa kuwachochea wanachama kusalitiana.
-
China, Afrika zaitaka Marekani kutatua mvutano wa kibiashara kwa mazungumzo yenye usawa
Jun 12, 2025 04:18Nchi 53 za Afrika pamoja na China zimeitaka Marekani kurejea kwenye meza ya mazungumzo ya kibiashara kwa msingi wa “usawa, heshima na manufaa ya pande zote”. Pia zimeihimiza kuachana na ushuru wa kulinda bidhaa za ndani na badala yake kuzingatia majadiliano ya kimataifa ya pande nyingi.
-
England yaangushwa kwa mara ya kwanza na timu ya Afrika
Jun 12, 2025 04:12Timu ya taifa ya Senegal imeandika historia kwa kuichapa England mabao 3-1 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa Jumanne mjini Nottingham, Uingereza.
-
WFP: Raia wa Kusini mwa Khartoum wanakabiliwa na tishio la njaa
Jun 11, 2025 22:44Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limeonya kuwa, maeneo kadhaa kusini mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum yamo hatarini kukumbwa na baa la njaa, kutokana na kuendelea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
-
Sudan yamtuhumu Haftar kwa kuunga mkono wanamgambo wa RSF
Jun 11, 2025 22:43Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Sudan imemtuhumu Khalifa Haftar mbabe wa kivita wa Libya kwa kuunga mkono mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF).
-
Rwanda: Nchi za Afrika zitumie teknolojia kuimarisha sekta ya kilimo
Jun 11, 2025 03:50Waziri Mkuu wa Rwanda ametoa mwito kwa nchi za Afrika kukumbatia teknolojia na ubunifu kupiga jeki sekta ya kilimo barani humo.
-
Afrika Kusini yazika miili 30 iliyotelekezwa kwenye mgodi wa dhahabu
Jun 11, 2025 03:49Afrika Kusini jana Jumanne ilifanya maziko ya kwanza ya 'kimaskini' ya miili 30 ambayo haikuchukuliwa na jamaa zao, baada ya kupatikana kwenye mgodi wa dhahabu uliotelekezwa huko Stilfontein, mkoa wa Kaskazini Magharibi mwezi Januari mwaka huu.