-
Waziri Mkuu wa Libya atoa amri ya kufanyika uchunguzi kuhusu mapigano ya Sabratha
Jun 06, 2025 23:00Waziri Mkuu wa Libya Abdul-Hamed Dbeibah jana Ijumaa alitoa amri kufanyika uchunguzi kuhusu mapigano yaliyozuka siku ya Alkhamisi katika mji wa pwani wa Sabratha wa kaskazini magharibi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Chad yasitisha utoaji wa visa kwa raia wa Marekani katika hatua ya kisasi
Jun 06, 2025 08:14Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby, siku ya Alhamisi alichukua hatua ya kujibu marufuku ya kusafiri iliyotangazwa na Marekani dhidi ya raia wa Chad, kwa kusitisha mara moja utoaji wa visa kwa raia wa Marekani.
-
UN yaelezea hofu yake kuhusu haki za binadamu Libya
Jun 06, 2025 03:18Umoja wa Mataifa umetaka uchunguzi huru ufanyike kuhusu mauaji ya kiholela yanayodaiwa kufanywa na kundi lenye silaha la Libya kufuatia kupatikana makumi ya maiti kwenye makaburi ya umati katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli.
-
Uchaguzi wa Bunge wafanyika Burundi, chama tawala chatarajiwa kuibuka na ushindi
Jun 05, 2025 09:05Wapiga kura nchini Burundi leo wameelekea katika vituo vya kupiga kura huku kukiwa na ongezeko la mfumuko wa bei, uhaba wa mafuta na malalamiko ya ukandamizaji wa kisiasa.
-
UN yataka uchunguzi wa makaburi ya halaiki yaliyogunduliwa Libya
Jun 05, 2025 03:23Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kufanyika uchunguzi huru na wa kina, baada ya kugunduliwa makaburi ya halaiki katika jela na vituo vya kuzuilia watu nchini Libya.
-
RSF yashambulia tena kambi ya wakimbizi na kuua 14 Darfur, Sudan
Jun 05, 2025 03:22Kwa akali watu 14 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi la mizinga la Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Zuma amkosoa Trump madai ya 'mauaji ya kimbari' Afrika Kusini, asema ni porojo tupu
Jun 04, 2025 22:45Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amemshutumu Rais wa Marekani Donald Trump kwa kile alichokiita "porojo zisizo na msingi", baada ya Trump kudai kwamba kuna mauaji ya kimbari yanayoendelea nchini Afrika Kusini.
-
Afrika yaendelea kusukuma juhudi za kupata Kiti cha Kudumu katika Baraza la Usalama la UN
Jun 04, 2025 22:42Bara la Afrika limeendeleza msimamo wake wa kutaka uwakilishi wa kudumu ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kufuatia kikao cha 13 cha Mawaziri wa Kamati ya Umoja wa Afrika ya Nchi Kumi (C-10), kilichofanyika Jumatano hii jijini Lusaka, mji mkuu wa Zambia.
-
UNHCR: Mgogoro mpya Sudan Kusini “umeng’oa” zaidi ya watu 165,000 ndani ya miezi mitatu
Jun 04, 2025 09:43Zaidi ya watu 165,000 wamelazimika kukimbia makazi yao na kukimbilia usalama wao maeneo mengi kutokana na mivutano na migogoro ambayo inazidi kuongezeka nchini Sudan Kusini katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
-
Wanajeshi wa Algeria waangamiza magaidi karibu na mpaka wa Tunisia
Jun 04, 2025 09:42Wizara ya Ulinzi ya Algeria imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limeangamiza magaidi wawili wenye silaha katika operesheni inayoendelea ya kukabiliana na magenge ya kigaidi katika mkoa wa mashariki wa Khenchela, karibu na mpaka wa nchi hiyo na Tunisia.