-
Kwa akali watu 109 wakiwemo watoto, wafariki dunia baada ya boti ya wahamiaji kupinduka karibu na pwani ya Djibouti
Oct 12, 2026 03:19Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limesema kuwa watu wasiopungua 109 wakiwemo watoto 15, wamefariki dunia baada ya boti iliyokuwa imebeba wahamiaji 305 kupinduka katika pwani ya Djibouti.
-
Jeshi la Ethiopia na washirika wake waripotiwa kuudhibiti mji wa mpakani na Eritrea
Oct 11, 2026 11:51Vikosi vya serikali ya Ethiopia na washirika wao vimeripotiwa kuingia kwenye mji wa Adigrat karibu na mpaka wa pamoja na jirani wa nchi hiyo wa Pembe ya Afrika, Eritrea.
-
Madaktari bingwa kutoka Tanzania wahitimisha kambi yao ya matibabu nchini Malawi
Oct 11, 2026 03:13Madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyoko mkoani Dodoma, Tanzania, wamehitimisha rasmi kambi yao ya matibabu nchini Malawi.
-
Kundi la RSF laua raia wengine jimboni Kordofan Kaskazini nchini Sudan
Oct 11, 2026 03:05Raia wanne wa familia moja wameuawa na wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka RSF katika jimbo la Kordofan Kaskazini nchini Sudan. Hayo yameripotiwa na kundi huru la kutetea haki za binadamu.
-
Watu 71 wauawa katika mapigano ya kijamii huko Rumbek, Sudan Kusini
Oct 10, 2026 11:41Serikali ya Sudan Kusini imetangaza kuwa, takriban watu 71, wakiwemo wanajeshi wameuawa katika mapigano ya kijamii kwenye Jimbo la Lakes la nchi hiyo.
-
Chanjo mpya ya Ebola yaanza kufanyiwa majaribio nchini Uganda
Oct 10, 2026 03:54Chanjo inayotarajiwa kutumika kupambana na virusi vya ugonjwa habari wa Ebola aina ya Bundibugyo imeingia katika hatua mpya ya majaribio ya kitabibu nchini Uganda, huku juhudi zikiongezeka za kuzalisha chanjo za virusi hivyo ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Ethiopia yatangaza kushinda vita, Shirika la Ndege kuanza tena safari kuelekea Tigray kesho Jumapili
Oct 10, 2026 03:50Shirika la Ndege la Ethiopia (Ethiopian Airlines) limetangaza kuwa litarejesha safari za ndege kuelekea Mekelle, makao makuu ya jimbo la Tigray, kuanzia tarehe 11 Oktoba baada ya vikosi vya serikali kuu kurejesha udhibiti wa mji huo Jumapili iliyopita.
-
Afrika Kusini: Magari 24 yachomwa moto huku maduka ya raia wa kigeni yakiporwa
Oct 09, 2026 09:44Takribani magari 24 yamechomwa moto na maduka yanayomilikiwa na raia wa kigeni kuporwa nchini Afrika Kusini, baada ya maandamano ya kupinga uhamiaji kugeuka kuwa vurugu katika miji ya Johannesburg na Durban.
-
Mashuhuda: Eritrea imepeleka askari wake eneo la Tigray ndani ya ardhi ya Ethiopia
Oct 08, 2026 10:52Wanajeshi wa Eritrea katika siku za karibuni wameingia kwenye eneo linalozunguka mji mmoja wa jimbo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, zikiwa zimepita wiki mbili tangu ulipoanza tena mzozo wa ndani nchini humo unaotishia kugeuka kuwa vita vya kikanda.
-
Umoja wa Afrika wazindua taasisi ya kutathmini uchumi wa nchi za bara hilo
Oct 08, 2026 03:17Umoja wa Afrika umezindua taasisi ya kwanza ya bara hilo ya kutoa daraja la sifa ya mikopo (credit rating agency), hatua inayolenga kuzipa nchi za Afrika njia mbadala ya taasisi tatu kubwa duniani: Moody’s, S&P Global na Fitch.