-
Mashuhuda: Eritrea imepeleka askari wake eneo la Tigray ndani ya ardhi ya Ethiopia
Oct 08, 2026 10:52Wanajeshi wa Eritrea katika siku za karibuni wameingia kwenye eneo linalozunguka mji mmoja wa jimbo la Tigray, kaskazini mwa Ethiopia, zikiwa zimepita wiki mbili tangu ulipoanza tena mzozo wa ndani nchini humo unaotishia kugeuka kuwa vita vya kikanda.
-
Umoja wa Afrika wazindua taasisi ya kutathmini uchumi wa nchi za bara hilo
Oct 08, 2026 03:17Umoja wa Afrika umezindua taasisi ya kwanza ya bara hilo ya kutoa daraja la sifa ya mikopo (credit rating agency), hatua inayolenga kuzipa nchi za Afrika njia mbadala ya taasisi tatu kubwa duniani: Moody’s, S&P Global na Fitch.
-
Ghana yatangaza azma ya kujiunga na kundi la kiuchumi la BRICS
Oct 08, 2026 03:12Ghana imesema itawasilisha rasmi ombi la kujiunga na kundi la kiuchumi la BRICS baada ya Baraza la Mawaziri la Rais John Dramani Mahama kuidhinisha hatua hiyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, amesema uamuzi huo ni sehemu ya juhudi za Ghana kupanua ushirikiano wake wa kimataifa na kutengeneza fursa zaidi za maendeleo ya kiuchumi.
-
Nigeria yatangaza maombolezo ya siku tatu baada ya wanajeshi 32 kufa kwenye ajali ya ndege
Oct 07, 2026 12:10Nigeria imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia jana Jumanne kwa ajili ya kuwalilia maafisa 32 wa Jeshi la Anga waliopoteza maisha wakati ndege ya kijeshi ilipoanguka katika Jimbo la Ondo la kusini-magharibi mwa nchi hiyo, juzi Jumatatu.
-
Jeshi la Mali lakomboa mji muhimu sana wa Kidal baada ya waasi kukimbia
Oct 07, 2026 12:06Jeshi la Mali limesema kuwa limefanikiwa kuukomboa na kuingia katika mji muhimu wa kimkakati wa Kidal wa kaskazini mwa nchi hiyo, ambao ulikuwa umetekwa mwezi Aprili na wanamgambo wanaotaka kujitenga wa kabila la Tuareg. Jana Jumanne wanamgambo hao walikimbia na jana na leo Jumatano jeshi la Mali limeingia mjini humo na kudhibiti kila kitu.
-
Marekani yaiingia tena mwilini Afrika Kusini
Oct 07, 2026 02:58Marekani imeanzisha mzozo mpya na Afrika Kusini na kupelekea kuzuka majibizano makali ya hadharani kati ya Waziri wa Afrika Kusini wa Masuala ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano, Ronald Lamola, na Balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Brent Bozell.
-
Kenya yathibitisha kifo cha kwanza cha mgonjwa wa Ebola
Oct 06, 2026 11:21Kenya imethibitisha kisa chake cha kwanza cha Ebola na kifo cha kwanza kinachohusishwa na ugonjwa huo nchini, humo baada ya raia wa Kenya aliyekuwa akiishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufariki muda mfupi baada ya kurejea Nairobi.
-
Jeshi la Ethiopia lasonga mbele Tigray, hofu yatanda katika ukanda mzima
Oct 06, 2026 03:29Jeshi la Taifa la Ulinzi la Ethiopia (ENDF) limeendelea kusonga mbele katika jimbo la Tigray lililokumbwa na mzozo, huku hofu ikiongezeka ya uwezekano wa mzozo huo kuenea katika nchi jirani na kuongezeka mvutano mkali wa kidiplomasia.
-
Viongozi wa nchi nne za Afrika watoa tamko la pamoja huku vita vikipamba moto nchini Ethiopia
Oct 05, 2026 10:46Misri, Eritrea, Somalia na Sudan zimetoa wito wa kutafutwa suluhisho la kisiasa na la njia za amani wakati mizozo inazidi kushtadi katika eneo la pembe ya Afrika, ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan na mapigano makali nchini Ethiopia.
-
Rais wa Somalia asema hawatakubali Israel iwepo katika ardhi ya nchi hiyo 'kwa hali yoyote ile'
Oct 05, 2026 03:39Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, ametangaza kuwa Somalia haitakubali uwepo wa jeshi la Israel katika ardhi yake "kwa hali yoyote ile", huku akionya kuwa Tel Aviv ina mpango wa kuanzisha kituo cha kijeshi cha majini katika eneo lililojitenga la Somaliland.