-
Mvua kubwa yauwa watu 2 na kujeruhi 40 katika mji wa Sabha, Libya
Sep 15, 2024 23:03Takriban watu wawili wamepoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika mji wa Sabha, kusini mwa Libya jana Jumapili.
-
Wanaharakati DRC wakaribisha kuhukumiwa kifo raia wa US
Sep 15, 2024 08:27Wanaharakati, wanasiasa na watetezi wa haki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameipongeza Mahakama ya Kijeshi ya nchi hiyo kwa kuwahukumu kifo watu 37 wakiwemo raia watatu wa Marekani na mmoja wa Uingereza, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na jaribio la kuipindua serikali katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika, Juni mwaka huu.
-
Wakulima 64 wafa maji katika ajali ya boti kaskazini ya Nigeria
Sep 15, 2024 04:01Watu wasiopungua 64 wanahofiwa kufa maji katika ajali ya boti iliyotokea mtoni katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.
-
Maambukizo ya ugonjwa wa Mpox yaongezeka nchini Uganda
Sep 15, 2024 03:57Idadi ya wagonjwa nchini Uganda walioambukizwa aina mpya ya virusi vya Mpox imeongezeka hadi 11, huku afisa mkuu wa afya akiripoti kuwa hakuna vifo vilivyosababishwa na maradhi hayo kufikia jana Jumamosi nchini humo.
-
Afrika Kusini: Tumedhamiria kuendelea na kesi yetu dhidi ya Israel ICJ
Sep 15, 2024 00:29Afrika Kusini imetangaza kuwa, imedhamiria kuendelea na kesi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), ambapo inaishutumu Israel kwa kufanya "mauaji ya halaiki" katika Ukanda wa Gaza.
-
Somalia yailalamikia Addis Ababa na kutishia kuwaunga mkono waasi wa Ethiopia
Sep 14, 2024 07:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Somalia, Ahmed Moalim Fiqi, amesema iwapo Ethiopia itaendelea mbele na makubaliano yake na kile alichokitaja kuwa waasi wa Somalia, nchi yake itakabiliana nayo kwa njia hiyo hiyo na kuanzisha uhusiano na waasi wa Ethiopia.
-
Raia wa Marekani, Uingereza wahukumiwa kifo DRC kwa jaribio la mapinduzi
Sep 14, 2024 04:00Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) siku ya Ijumaa iliwahukumu kifo watu 37 wakiwemo raia watatu wa Marekani kwa kuhusika katika jaribio la kuipindua serikali hiyo ya kati mwa Afrika mapema mwaka huu.
-
Sudan Kusini yaahirisha uchaguzi, yaongeza muda wa serikali ya mpito kwa miaka miwili
Sep 14, 2024 03:55Sudan Kusini imeahirisha uchaguzi wake uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu hadi Desemba 2026, kutokana na udhaifu wa mchakato wa amani katika nchi hiyo changa zaidi duniani.
-
Kaimu Mkuu wa Polisi nchini Kenya ahukumiwa kifungo cha miezi sita jela
Sep 14, 2024 00:58Kaimu Mkuu wa Polisi nchini Kenya Ijumaa ya jana alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukaidi mara kwa mara amri ya kutoa ushahidi kuhusu mahali walipo watu watatu ambao wametoweka baada ya kudaiwa kukamatwa na maafisa wa polisi.
-
Rais wa Senegal avunja bunge, aitisha uchaguzi wa mapema Novemba
Sep 13, 2024 08:12Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye amelivunja bunge la nchi hiyo linaloongozwa na upinzani na kuitisha uchaguzi wa mapema ili kumaliza mvutano kati ya bunge na serikali.