Sep 15, 2024 07:31 UTC
  • Wakulima 64 wafa maji katika ajali ya boti kaskazini ya Nigeria

Watu wasiopungua 64 wanahofiwa kufa maji katika ajali ya boti iliyotokea mtoni katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Boti ya mbao iliyokuwa na wakulima 70 ilipinduka ilipokuwa ikiwasafirisha kuvuka mto hadi kwenye mashamba yao karibu na mji wa Gummi Jumamosi asubuhi.

Mamlaka za eneo hilo zilihamasisha na kuwakusanya wakazi wa eneo hili haraka na kuanzisha operesheni ya uokoaji, na baada ya saa tatu, manusura sita pekee ndio waliokolewa kutoka majini.

Hili ni tukio la pili katika eneo la Gummi, kwa mujibu wa Aminu Nuhu Falale, msimamizi wa eneo hilo ambaye aliongoza juhudi za uokoaji.

Afisa huyo wa serikali za mitaa amebainisha kuwa, timu za dharura zinaendelea na msako wao kwa matumaini ya kupata manusura zaidi.

Zaidi ya wakulima 900 wanategemea kuvuka mto huo kila siku ili kufikia mashamba yao, lakini ni boti mbili tu zinazopatikana, mara nyingi husababisha msongamano, amesema mtawala wa jadi wa eneo hilo.

Tags