-
Algeria yatangaza iko tayari kutuma jeshi Gaza kusaidia Wapalestina
Aug 19, 2024 08:35Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupeleka wanajeshi katika Ukanda wa Gaza kuwasaidia Wapalestina wa eneo hilo punde tu mipaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza itakapofunguliwa.
-
Sudan yatuma wajumbe mjini Cairo kukutana na wapatanishi
Aug 19, 2024 08:32Serikali ya Sudan imetuma wajumbe wake mjini Cairo kwa majadiliano juu ya ushiriki wake katika mazungumzo ya amani yenye lengo la kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miezi 16 nchini humo.
-
Afrika Kusini yawatimua Walibya 95 waliokamatwa katika kambi haramu ya mafunzo ya kijeshi
Aug 19, 2024 02:40Afrika Kusini jana Jumapili iliwatimua raia 95 wa Libya ambao walikamatwa mwezi uliopita katika kambi ya siri inayoshukiwa ni ya kijeshi katika jimbo la Mpumalanga la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
-
Algeria kuharakisha kupeleka mafuta Lebanon ili kupunguza mgogoro wa umeme
Aug 19, 2024 02:39Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria ameamuru kupelekwa haraka mafuta nchini Lebanon ambayo imekumbwa na uhaba mkubwa wa umeme.
-
Rais wa Zimbabwe atoa mwito wa kufanyika juhudi za kuhifadhi historia ya Afrika
Aug 19, 2024 02:39Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana Jumapili alizitaka nchi za Afrika kuhakikisha kwamba historia ya bara hilo imeandikwa kwa usahihi na kulindwa ili kuzuia dosari za kihistoria.
-
Abdul-Fatah al-Burhan kuunda serikali ya mpito Sudan
Aug 18, 2024 23:21Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan ametangaza habari ya kuweko juhudi za kuunda serikali ya mpito katika nchi hiyo inayosumbuliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
-
Miripuko pacha ya mabomu yaua watu kadhaa mjini Mogadishu, Somalia
Aug 18, 2024 08:43Kwa akali watu wanane wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika miripuko pacha ya mabomu iliyotokea katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
-
Sudan yatangaza janga la kipindupindu baada ya mvua kubwa kunyesha nchini humo
Aug 18, 2024 03:34Waziri wa Afya wa Sudan ametangaza janga la kipindupindu nchini humo baada ya mvua kubwa kunyesha kwa wiki kadhaa.
-
SADC: Watu milioni 68 wanasumbuliwa na ukame kusini mwa Afrika
Aug 18, 2024 03:32Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) imesema makumi ya mamilioni ya watu wameathiriwa na ukame uliosababishwa na El Nino katika eneo la Kusini mwa Afrika, na wanahitaji msaada wa haraka wa chakula.
-
Udhalilishaji wa kingono watumiwa kama silaha ya vita katika mzozo huko Sudan
Aug 17, 2024 22:58Pande husika katika vita vya ndani nchini Sudan zimetekeleza udhalilishaji wa kingono na vitendo vingine vya unyanyasaji kama silaha ya vita tangu kuanza mapigano ya ndani nchini humo mwezi Aprili mwaka jana.