-
UN yarefusha muda wa vikosi vya AU kuhudumu Somalia hadi Desemba mwaka huu
Aug 17, 2024 06:03Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha Azimio nambari 2748, linaloruhusu mamlaka ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) kusalia nchini humo hadi Desemba mwaka huu.
-
Watu 80 wauawa nchini Sudan katika shambulio la kikosi cha RSF
Aug 17, 2024 03:40Kwa akali watu 80 wameuawa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na kikosi cha Usaidizi wa Haraka RSF katika kijiji cha kusini mashariki mwa nchi hiyo. Hayo yameelezwa na chanzo kimoja nchini humo.
-
Wanafunzi 20 wa vyuo vikuu watekwa nyara nchini Nigeria
Aug 17, 2024 03:39Wanafunzi wapatao 20 wa vyuo vikuu vya Nigeria wametekwa na watu wenye silaha waliovizia magari yao kaskazini mwa nchi hiyo.
-
UNICEF yaonya kuhusu hali mbaya ya watoto nchini Sudan
Aug 17, 2024 00:54Watoto nchini Sudan wanateseka kwa hali mbaya inayozidi kuwa hatarishi huku vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi vikiendelea bila ya kuonesha dalili za kupungua. Mbali na hayo, mgogoro wa hali ya hewa nao unaweza kusababisha makumi ya maelfu ya vifo vya watoto katika miezi ijayo huko Sudan.
-
Watu 16 wauawa katika makabiliano baina ya waasi, wanamgambo DRC
Aug 16, 2024 07:40Mapigano kati ya waasi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamepelekea kuuawa wanakijiji 16.
-
Mafuriko yaua zaidi ya watu 50 kaskazini mwa Chad
Aug 16, 2024 07:09Watu wasiopungua 54 wamefariki dunia kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika jimbo la Tibesti la kaskazini mwa Chad.
-
Polisi Kenya watuhumiwa; Walikuwa wakijua uhalifu uliofanyika Shakahola, asema shahidi
Aug 16, 2024 04:02Maafisa usalama walikuwa na nafasi ya kuepusha maafa ya vivyo vya zaidi ya watu 400 Shakahola iwapo wangefuatilia kwa undani ripoti za uvamizi wa eneo hilo mwaka wa 2021.
-
Umoja wa Mataifa wahuzunishwa na hatua mbaya za makundi ya Libya
Aug 16, 2024 00:44Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL umeelezea kuhuzunishwa kwake na hatua za upande mmoja za hivi karibuni za pande hasimu na baadhi ya vyama vya siasa nchini humo.
-
Rwanda yatia saini makubaliano ya ujenzi wa vinu vya nyuklia
Aug 15, 2024 09:26Rwanda imetangaza kuwa, imetia saini mkataba wa maelewano na kampuni ya Kimarekani ya Nano Nuclear Energy kwa ajili ya ujenzi wa vinu vidogo vya nyuklia (SMR). Tangazo hilo limetolewa na Mamlaka ya Nishati ya Atomiki ya Rwanda (RAEB).
-
UN:80% ya Wasudan Kusini wanahitaji ulinzi, msaada wa kibinadamu
Aug 14, 2024 23:15Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayozidi kuzorota nchini Sudan Kusini, huku takriban asilimia 80 ya wananchi wa nchi hiyo wakihitaji kudhaminiwa usalama na ulinzi na vile vile kupewa msaada wa kibinadamu.