Algeria yatangaza iko tayari kutuma jeshi Gaza kusaidia Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i115412-algeria_yatangaza_iko_tayari_kutuma_jeshi_gaza_kusaidia_wapalestina
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupeleka wanajeshi katika Ukanda wa Gaza kuwasaidia Wapalestina wa eneo hilo punde tu mipaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza itakapofunguliwa.
(last modified 2024-08-19T08:35:38+00:00 )
Aug 19, 2024 08:35 UTC
  • Algeria yatangaza iko tayari kutuma jeshi Gaza kusaidia Wapalestina

Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune ametangaza kuwa jeshi la nchi yake liko tayari kupeleka wanajeshi katika Ukanda wa Gaza kuwasaidia Wapalestina wa eneo hilo punde tu mipaka kati ya Misri na Ukanda wa Gaza itakapofunguliwa.

Katika hotuba yake katika siku ya nne ya kampeni za uchaguzi katika Constantine kaskazini mashariki mwa Algeria, Tebboune ameongeza kuwa: "Hatutaiacha kamwe Palestina, hasa Gaza", na kuongeza, "Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ikiwa wataturuhusu na kufungua mipaka kati ya Misri na Gaza... basi kuna kitu tunaweza kufanya.”

Tebboune ambaye anatetea kiti chake katika uchaguzi ujao wa rais Septemba 7, aliendelea kusema, "Nilitoa ahadi na jeshi liko tayari mara tu mipaka itakapofunguliwa na lori zetu kuruhusiwa kuingia, ndani ya siku 20 tutajenga hospitali tatu, tutapeleka mamia ya madaktari, na kusaidia kujenga upya kile ambacho Wazayuni wameharibu. "

Rais wa Algeria ameeleza mara kadhaa uungaji mkono kamili wa nchi yake kwa kadhia ya Palestina na kusisitiza kuwa ukombozi wa Palestina ni kadhia tukufu.