-
Rais Kagame ahifadhi kiti chake, ashinda uchaguzi kwa 99%
Jul 16, 2024 03:50Matokeo ya awali ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) yanaonyesha kuwa, Rais Paul Kagame yuko kifua mbele kwa kuzoa asilimia 99.15 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa rais uliofanyika jana Jumatatu.
-
Mapigano baina ya jeshi na wanamgambo yaua watu 50 DRC
Jul 16, 2024 03:49Watu zaidi ya 50 wameripotiwa kuuawa katika mapigano makali baina ya askari wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi moja la wanamgambo magharibi mwa nchi.
-
Ruto: Wakfu wa US ndio unaochochea maandamano ya fujo Kenya
Jul 15, 2024 23:44Rais William Ruto wa Kenya ameujia juu Wakfu wa Ford wa Marekani, akiuhusisha na vurugu zilizoshuhudiwa nchini humo wakati wa maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 na jinsi utawala wa Kenya Kwanza unaendesha serikali.
-
Uganda kuwa mwenyeji wa kongamano la 11 la utawala wa kimtandao wa Afrika Mashariki
Jul 15, 2024 23:24Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetangaza katika taarifa yake ya jana Jumatatu kwamba, Uganda itakuwa mwenyeji wa Kongamano la 11 la Utawala wa Kimtandao wa Afrika Mashariki (EAIGF) kwa ajili ya kushughulikia masuala muhimu ambayo yataboresha matumizi ya Intaneti katika masuala ya kiutawala kwenye ukanda huo mzima.
-
Maelfu ya watu wanateseka baada ya kukimbia mapigano katikati mwa Sudan
Jul 15, 2024 23:23Takwimu za mamlaka husika zinaonesha kuwa makumi ya maelfu ya watu wanateseka hivi sasa baada ya kukimbia mapigano katika jimbo la Sinnar la katikati mwa Sudan. Watu hao wamekimbilia kwenye jimbo la Gedaref baada ya kushadidi mapigano ya uchu wa madaraka kati ya majenerali wa kijeshi wanaoongoza makundi mawili ya RSF na SAF.
-
Jeshi la Sudan: Tumeua zaidi ya wanamgambo 100 wa RSF mjini Khartoum
Jul 15, 2024 09:45Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kuwa, limeua zaidi ya wapiganaji 100 wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na kujeruhi makumi ya wengine wakati wa operesheni maalumu ya jeshi hilo katika mji mkuu Khartoum, siku ya Jumamosi pekee.
-
Atiwa mbaroni baada ya kukiri kuua wanawake 42 Kenya
Jul 15, 2024 08:14Polisi nchini Kenya imemkamata mshukiwa wa mauaji ya makumi ya wanawake viungani mwa mji mkuu, Nairobi.
-
25 wauawa, kujeruhiwa Somalia wakitazama fainali ya EURO 2024
Jul 15, 2024 07:23Kwa akali watu watano wameuawa huku makumi ya wengine wakijeruhiwa katika shambulio la bomu linaloaminika kufanywa na kundi la kigaidi la al-Shabaab huko Mogadishi, mkuu wa Somalia.
-
Miili zaidi yagunduliwa kwenye magunia Nairobi, taharuki yatanda
Jul 15, 2024 04:20Kugunduliwa mili zaidi ya watu ikiwa imefungwa kwenye magunia jijini Nairobi nchini Kenya kumezidisha taharuki na kuibua kitendawili cha nani amehusika na vifo au muaji hayo.
-
Gavana wa Khartoum: Maelfu ya wageni wanapigana katika safu za RSF dhidi ya serikali ya Sudan
Jul 15, 2024 03:30Gavana wa Jimbo la Khartoum, Ahmed Othman Hamza, amefichua kwamba mamlaka ya serikali imewataka wageni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria kuondoka na kurejea katika nchi zao baada ya maelfu yao kuhusika katika mapigano ya ndani wakishirikiana na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) dhidi ya jeshi la taifa.