-
Kupasishwa mpango wa kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Niger
Jul 06, 2024 03:18Baada ya miezi minne, serikali ya Marekani imetangaza kwamba vikosi vyake vyote vya kijeshi vitaondoka nchini Niger hivi karibuni.
-
Ruto achukua hatua za kubana matumizi kufuatia maandamano ya vijana
Jul 05, 2024 23:09Katika hatua za kubana matumizi, Rais William Ruto wa Kenya ametangaza kwamba atapunguza idadi ya washauri wa serikali kwa asilimia 50, huku watumishi wa umma waliofikisha umri wa kustaafu (miaka 60) wakitakiwa kuondoka kazini mara moja.
-
Takriban wahamiaji 89 wamefariki dunia baada ya mtumbwi kupinduka pwani ya Mauritania
Jul 05, 2024 23:06Mtumbwi mmoja uliokuwa na wahamiaji haramu umepinduka katika fukwe za Mauritania na kusababisha vifo vya wahamiaji 89. Mtumbwi huo ulikuwa unaelekea barani Ulaya na watu walioshuhudia wanasema kuwa, ulikuwa na abiria 170.
-
Watu 25 wafa maji katika hamkani za kukimbia vita nchini Sudan
Jul 05, 2024 06:49Takriban watu 25 wamekufa maji kusini mashariki mwa Sudan walipokuwa wakijaribu kukimbia mapigano ya uchu wa madaraka kati ya jeshi la Sudan SAF na Viikosi vya Msaada wa Haraka RSF.
-
Askari wa SADC wahitimisha operesheni dhidi ya ugaidi kaskazini mwa Msumbiji
Jul 05, 2024 06:48Kikosi cha Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika nchini Msumbiji (SAMIM) kimetangaza kuwa, kimeamua kuondoka katika jimbo la Cabo Delgado la kaskazini mwa Msumbiji ikiwa ni kiashirio kwamba kikosi hicho kimefanikiwa kurejesha usalama na amani jimboni humo.
-
Al-Burhan: Wanamgambo wa Daesh wanapigana katika Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)
Jul 05, 2024 03:58Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kuwa wanamgambo wa kundi la Daesh wanapigana katika safu ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyoongozwa na Muhammad Hamdan Dagalo (Hemedti), akisisitiza kuwa jeshi la Sudan linapinga makubaliano yoyote ambayo hayatanguliwi na kuondolewa kwa vikosi vya RSF katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.
-
Raia 6 wa China na askari 2 wa DRC wauawa mkoani Ituri
Jul 04, 2024 22:46Waasi wa kundi la CODECO wameshambulia mgodi unaohusishwa na China katika jimbo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua raia sita wa China wa wanajeshi wawili wa Kongo.
-
Watu milioni 66 wanakabiliwa na uhaba wa chakula Pembe ya Afrika
Jul 04, 2024 22:43Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Jumuiya ya Kiserikali ya Maendeleo ya Afrika Mashariki IGAD zimesema katika ripoti yao mpya kwamba, watu milioni 66.7 katika eneo pana la Pembe ya Afrika hawana usalama wa chakula.
-
Mapigano yaendelea Sudan huku juhudi za kuwakutanisha majenerali hasimu zikifeli
Jul 04, 2024 08:42Mapigano kati ya jeshi na kikosi cha msaada wa haraka yameshadidi tena nchini Sudan huku juhudi za kuwakutanisha majerali hasimu nchini huumo zikigonga mwamba.
-
Human Rights Watch: Vikosi vya Ethiopia vimetenda jinai za kivita Amhara
Jul 04, 2024 08:41Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limetangaza kuwa, vikosi vya Ethiopia vimefanya jinai za kivita katika eneo la Amhara.