Kupasishwa mpango wa kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini Niger
Baada ya miezi minne, serikali ya Marekani imetangaza kwamba vikosi vyake vyote vya kijeshi vitaondoka nchini Niger hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, serikali ya Marekani ilitangaza kwamba hivi karibuni itaondoa vikosi vyake vyote vya kijeshi kutoka Niger baada ya kuakhirisha kuondoka kwa vikosi vyake vya kijeshi kutoka Niger.

Katika mahojiano na CBS, Jenerali Kenneth Ackman, mmoja wa makamanda wa Jeshi la Anga la Marekani, alisema kwamba baadaye wiki hii, wanajeshi wa Marekani waliopo katika "kambi ndogo" wataondoka Niger, na kisha mwezi Agosti, wanajeshi wengine 500 wa Marekani waliopo katika nchi hiyo wataondoka katika kituo kikuu cha usimamizi cha Niger.
Kambi hiyo ya ndege zisizo na rubani, inayojulikana kama "Niger Air Base 201", ilikabiliwa na makelele mengi na ilisemekana kuwa ni kituo kikuu cha shughuli za kijasusi cha Huduma ya Siri ya Marekani (CIA).
Na mwishoni mwa mwezi Machi, 2024, baraza tawala nchini Niger lilifuta makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi na Washington na kuzingatia kuwepo kwa wanajeshi wa Marekani nchini Niger kuwa ni kinyume cha sheria na kinyume na maslahi ya nchi hiyo.
Kuhusiana na suala hilo, Amadou Abdel Rahman, msemaji wa baraza la uongozi la Niger, alitoa taarifa na kusema kwamba; "Serikali ya Niger, kwa kuzingatia maadili na maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo, iliamua kufuta kwa upande mmoja mkataba wake wa kijeshi na Marekani.