-
Al Burhan akataa pendekezo la Marekani, alitaja kuwa baya zaidi kwa ajili ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan
Nov 24, 2025 11:54Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amekataa pendekezo lililowasilishwa na mshauri wa Rais wa Marekani kuhusu masuala ya Kiarabu na Afrika, Massad Boulos, juu ya utatuzi wa mgogoro wa Sudan.
-
Tanzania kuanza kujenga bandari yenye thamani ya dola bilioni 10 mwezi Desemba
Nov 24, 2025 11:44Tanzania itaanza ujenzi wa bandari mpya mashariki mwa nchi mwezi Desemba mwaka huu na hivyo kumaliza muongo mmoja wa ucheleweshaji kutokana na pingamizi la serikali kwa masharti ya awali ya kandarasi.
-
Raia wengi wakimbia makazi yao baada ya magaidi kuteka nyara mabinti 13 katika jamii ya Borno, Nigeria
Nov 24, 2025 11:09Wimbi la hofu limeikumba jamii ya Borno, na raia wengi wameanza kuondoka majumbani mwao leo Jumatatu, siku mbili baada ya ISWAP, tawi la kundi Boko Haram, kuwateka nyara mabinti 13 wenye umri wa miaka 15 hadi 20.
-
Wanafunzi 50 kati ya 300 waliotekwa Nigeria wafanikiwa kutoroka
Nov 24, 2025 03:41Wanafunzi 50 kati ya 300 waliotekwa nyara na watu waliojihami kwa silaha kwenye jimbo la katikati mwa Nigeria la Niger, wamefanikiwa kuwatoroka watekaji wao.
-
Guterres: Afrika itagharamika pakubwa licha ya kuchangia kidogo sana mabadiliko ya tabianchi
Nov 23, 2025 23:50Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema kuwa Afrika italipa "gharama kubwa" kutokana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi licha ya kuhusika kwake kwa kiwango kidogo sana katika mabadiliko hayo.
-
Tanzania yazionya BBC, CNN, DW na al-Jazeera ikisema vina nia ovu
Nov 23, 2025 23:48Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amevikosoa vyombo vya habari vya nje akivitaka kufuata maadili na misingi ya uandishi wa habari.
-
Kwa nini ugonjwa wa kichaa cha mbwa unaua maelfu barani Afrika licha ya kuwa unaoweza kuzuilika?
Nov 23, 2025 23:33Ulimwenguni kote, kichaa cha mbwa huua takriban watu 59,000 kila mwaka, na karibu 95% ya vifo hivi vikitokea Afrika na Asia. Hii inasababishwa na ongezeko la idadi ya mbwa wanaotangatanga bila chanjo, upatikanaji duni wa matibabu na kushindwa kutolewa taarifa ya ugonjwa huu kwa wakati.
-
Jeshi la Sudan lakabiliana vikali na kikosi cha RSF huko Kordofan; raia wazidi kutaabika
Nov 23, 2025 09:33Jeshi la Sudan limekabiliana vikali mapiganoni dhidi ya wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) katika medani tofauti za vita huko Kordofan ya Kaskazini na Magharibi huku makumi ya maelfu ya raia wakiendelea kukimbia machafuko na mapigano yanayoshtadi kila uchao.
-
Global Citizen: Mkutano wa G20 umefikia malengo licha ya mivutano
Nov 23, 2025 08:56Afrika Kusini imefikia malengo muhimu katika mkutano wa kilele wa kundi la mataifa tajiri na yale yanayoinukia kiuchumi duniani G20 licha ya mivutano ya kimataifa. Hayo yameelezwa na shirika la hisani la Global Citizen.
-
Wanafunzi 303, walimu 12 watekwa nyara na watu wenye silaha katika skuli ya jimbo la Niger, Nigeria
Nov 23, 2025 03:03Jumuiya ya Wakristo ya Nigeria (CAN) imetangaza kuwa, jumla ya wanafunzi 303 na walimu 12 wametekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana likiwa ni tukio la pili kubwa kutokea ndani ya wiki moja, huku hofu za usalama zikiongezeka katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.