-
Magaidi 200 wauawa katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi nchini Nigeria
Nov 10, 2025 23:26Mapigano kati ya makundi hasimu ya kigaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha vifo vya magaidi wasiopungua 200 katika eneo la Ziwa Chad.
-
Binti wa Zuma akana mashtaka ya uchochezi
Nov 10, 2025 23:22Duduzile Zuma-Sambudla, bintiye rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, amekana mashtaka ya kuchochea ghasia wakati wa machafuko makubwa yaliyotokea nchini humo mwezi Julai 2021.
-
Hatari ya ushawishi wa Israel barani Afrika; Tishio lililofichika kwa uhuru wa bara Afrika
Nov 10, 2025 09:35Katika juhudi zake za kuitoa Israel kwenye hali ya kutengwa, Isaac Herzog, rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel, anatarajiwa kuelekea barani Afrika.
-
Gavana wa Darfur: Al Burhan aamuru vikosi kusonga mbele kuelekea magharibi
Nov 10, 2025 08:43Gavana wa Darfur na kiongozi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan, Minni Arko Minnawi amesema kwamba mkuu wa Baraza la Utawala na kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, ameamuru kusonga mbele kuelekea magharibi mwa Darfur.
-
AU yatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kimataifa kushughulikia mgogoro wa Mali
Nov 10, 2025 07:30Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssef, ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuzorota kwa kasi hali ya usalama nchini Mali, ambako makundi aliyoyataja kuwa ya "kigaidi" yamezuia operesheni za kuwasilisha mahitaji ya msingi na hivyo kuzidisha mgogoro wa binadamu unaowakabili raia, pamoja na kuongezeka kwa utekaji nyara.
-
RSF imezika kwa halaiki na kuchoma moto maiti za mamia ya raia El-Fasher kuficha jinai za mauaji ya kimbari
Nov 10, 2025 02:48Mtandao wa Madaktari wa Sudan umeripoti kuwa, maiti za mamia ya raia zimezikwa katika makaburi ya pamoja na nyingine zimechomwa moto na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) mjini El-Fasher magharibi mwa nchi hiyo.
-
Minawi aonya dhidi ya kugawanyika tena Sudan
Nov 09, 2025 22:51Gavana wa Darfur, Minni Arko Minnawi, ameonya kwamba makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano nchini Sudan ambayo hayajumuishi ulinzi wa raia na kuwajibishwa wahusika wa uhalifu "yatakuwa na maana ya mgawanyiko wa Sudan," na ametoa wito wa kuondoka wale aliowaita "Janjaweed na mamluki" - akikusudia Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF)- katika maeneo ya makazi ya raia, hospitali na mijini.
-
Magaidi watatu vinara wa al-Shabaab wauawa katika operesheni ya jeshi la Somalia
Nov 09, 2025 22:50Jeshi la Somalia jana Jumapili lilifanya oparesheni kadhaa katika majimbo ya Bakool na Bay na kuuwa wanachama wa ngazi ya juu wa kundi la kigaidi la al Shabaab.
-
Mtandao wa Madaktari Sudan: RSF imeteketeza mamia ya miili ya watu huko El Fasher
Nov 09, 2025 06:34Mtandao wa Madaktari wa Sudan umesema kwamba Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vilikusanya mamia ya miili kutoka mitaani na vitongoji vya makazi ya raia vya El Fasher (mji mkuu wa Darfur Kaskazini) na kuzika baadhi ya miili hiyo katika makaburi ya umati, huku mingine ikichomwa moto kabisa.
-
Maandamano yazuka Nigeria kufuatia tishio la Trump la kuivamia nchi hiyo kijeshi
Nov 09, 2025 03:48Wananchi walimiminika mitaani siku ya Jumamosi katika jiji la Kano, kaskazini mwa Nigeria, kupinga vitisho vya Rais Donald Trump wa Marekani, vya kuivamia nchi hiyo kijeshi.