-
Operesheni ya kijeshi ya Iran ya Ahadi ya Kweli-3 yasababisha uharibifu mkubwa Tel Aviv na Haifa
Jun 22, 2025 11:33Wimbi jipya la mashambulio ya makombora ya Iran ya operesheni ya Ahadi ya Kweli-3 limesababisha uharibifu mkubwa katika miji ya Tel Aviv na Haifa.
-
Taarifa ya Iran kuhusu uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya vituo vya amani vya nyuklia vya Iran
Jun 22, 2025 07:17Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imetoa taarifa ikilaani hujuma na uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya taifa hili vinavyofanya shughuli zake kwa malengo ya amani.
-
Mohammad Eslami: Hatuamini tena wakala wa IAEA na ukaguzi wake
Jun 22, 2025 07:06Mohammad Eslami Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa, hatuna imani tena na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na ukaguzi wake, kwa sababu zana zote hizo zimetumika katika kufanya ujasusi kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Spika Qalibaf: Utawala wa Kizayuni umechafua tena mikono yake kwa jinai mpya kwa idhini ya Marekani
Jun 16, 2025 09:03Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amebainisha kuwa, utawala haramu wa umechafua mikono yake michafu kwa jinai mpya kwa idhini ya Marekani na kueleza kuwa, "watu wa Iran, wa kila kabila na mirengo tofauti ya kisiasa, wameungana na kuwa kitu kimoja dhidi ya adui katili, na bila shaka walimwengu watashuhudia adhama ya Iran na Wairani."
-
Rais wa Iran: Ni lazima tuungane dhidi ya uchokozi wa utawala wa kijinai wa Israel
Jun 16, 2025 07:51Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian amesema wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu wanahitaji umoja na mshikamano wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule, na lazima washikane mikono na kusimama kidete kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Israel unaofanya mauaji ya kimbari.
-
Israel yashambulia hospitali ya watoto Tehran na kuua shahidi kadhaa
Jun 16, 2025 07:50Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei ameulaani vikali utawala haramu wa Israel kwa kuwaua shahidi watoto katika vita vyake vya kichokozi vinavyoendelea dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran yamyonga jasusi wa Mossad; msako dhidi ya maajenti wengine unaendelea
Jun 16, 2025 06:25Iran mapema leo imetekeleza hukumu ya kumnyonga Esmail Fekri, jasusi aliyepatikana na hatia ya kushirikiana na shirika la kijasusi la Israel la Mossad.
-
Uhalifu wa Kivita: Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran lalengwa katika hujuma ya Israel
Jun 16, 2025 04:17Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali shambulizi la kigaidi la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya moja ya majengo yake katika mji mkuu, Tehran.
-
Jeshi la Iran lawaonya walowezi Waisraeli: Ondokeni muokoe maisha yenu
Jun 16, 2025 04:12Majeshi ya Iran yametoa onyo kali kwa walowezi Waisraeli walio katika maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu (Israel) na kuwataka waondoke mara moja, huku Iran ikijiandaa kutekeleza mashambulizi makubwa yanayotarajiwa kuenea katika ardhi zote zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Iran yagundua na kusambaratisha karakana ya Mossad ya kuunda droni karibu na Tehran
Jun 16, 2025 04:04Maafisa wa usalama wa Iran wamevamia makazi ya ghorofa tatu nje kidogo ya Tehran, ambapo wamegundia kituo cha siri kinachoendeshwa na shirika la kijasusi la Israel, Mossad, kwa ajili ya kuunganisha droni na vilipuzi.