-
UN: Tuna hamu ya kushirikiana na Rais mpya wa Iran
Jul 09, 2024 04:24Stephane Dujarric Msemaji wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa taasisi hiyo ya kimataifa ina hamu ya kushirikiana na Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian.
-
Pezeshkian: Kuunga mkono muqawama ni katika sera kuu za Iran
Jul 08, 2024 23:38Rais mteule wa Iran amesema serikali yake ijayo itafanya kile iwezalo kuunga mkono vikosi vya muqawama katika eneo la Asia Magharibi, akisisitiza kuwa kuuunga mkono mrengo wa mapambano ni katika sera kuu za Jamhuri ya Kiislamu.
-
Kanani: Marekani iheshimu demokrasia ya kidini nchini Iran
Jul 08, 2024 22:56Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja msimamo wa serikali ya Marekani kuhusu uchaguzi kuwa wenye kudhihirisha kiwango cha uingiliaji wa siasa mbovu za nchi hiyo mkabala wa Iran na kusema: Inatarajiwa kuwa Marekani itaheshimu demokrasia ya kidini nchini Iran.
-
Ghuba ya Uajemi; nembo ya ukweli wa kihistoria usiokanushika
Jul 08, 2024 22:53Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akijibu msimamo wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kuhusiana kuheshimiwa ardhi yote ya Iran na kutopotoshwa jina la Ghuba ya Uajemi.
-
Iran yawalaumu vikali wanaouunga mkono utawala wa Kizayuni
Jul 08, 2024 07:35Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, ni aibu kwa nchi na mtu yoyote kuunga mkono jinai za utawala wa Kizayuni huko Ghaza na aibu hiyo haitofutika milele kwenye vipaji vya nyuso zao.
-
Jumbe za uchaguzi wa rais wa Iran kwa nchi za eneo
Jul 08, 2024 03:12Duru ya pili ya uchaguzi wa 14 wa rais wa Iran ilifanyika Ijumaa iliyopita ya Julai 5 na Masoud Pezeshkian amechaguliwa kuwa rais wa 9 wa Iran.
-
Kiongozi wa Mapinduzi: Shahid Raisi, ni kigezo cha uongozi kwa serikali na viongozi
Jul 07, 2024 09:13Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, ametaja juhudi zisizokoma za kutatua matatizo ya watu, imani kubwa juu ya uwezo wa ndani, kuwa wazi katika kutangaza misimamo ya kidini na kimapinduzi, kutochoka, kutokata tamaa, kujitolea katika utekelezaji wa mipango mikubwa, unyenyekevu na uvumilivu na kushikamana na masuala ya kiroho, dhikri na kutawasali kuwa nii miongoni mwa sifa bora za kibinafsi, kimienendo na za kikazi za Shahid Ebrahim Raisi.
-
Nukta muhimu katika ujumbe wa Kiongozi Muadhamu kwa kikao cha Umoja wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya
Jul 07, 2024 08:23Katika ujumbe wake kwa mkutano wa 58 wa Jumuiya za Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, ameashiria masuala tata ya hivi sasa ya ulimwengu na akasisitiza nafasi na taathira za wanafunzi hao katika masuala makubwa kwa kuegemea shauku, imani na kujiamini.
-
Balozi wa Iran UN awasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama kufuatia madai yasiyo na msingi ya Arab League
Jul 07, 2024 04:11Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu madai ya uwongo yaliyotolewa na Jumuia ya Nchi za Kiarabu kuhusu Iran.
-
EU: Tuko tayari kuboresha ushirikiano na Iran
Jul 07, 2024 04:07Msemaji wa Umoja wa Ulaya anayehusika na sera ya mambo ya nje na usalama amempongeza Rais mteule wa Iran na kusema umoja huo uko tayari kustawisha ushirikiano wa pande mbili na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.