Sep 14, 2024 04:38 UTC
  • Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa: Hali ya mambo ya Gaza ni kashfa kubwa zaidi ya kihistoria

Waziri Mkuu wa zamani wa Ufaransa ametaja hali ya mambo huko Gaza kuwa ni "kashfa kubwa zaidi ya kihistoria" na kukosoa msimamo wa Ufaransa kuhusu vita vinavyoendelea katika eneo hilo.

Dominique de Villepin ameiambia kanali ya habari ya France Inter kuwa na hapa ninamnukuu: 'Hatuna sauti tena katika ngazi ya kimataifa; raia wa kawaida wanapoteza maisha kila siku huko Gaza, hali ya Gaza ni kashfa ya kweli katika suala la demokrasia." Mwisho wa kunukuu.   

Dominique de Villepin ambaye alihudumu kuanzia mwaka  2005 hadi 2007, kama Waziri Mkuu wa Ufaransa amelaani mauaji ya raia na kusema miili, mioyo  na vichwa vya raia wa Ukanda wa Gaza vimeshuhudiwa vikiwa vipande vipande katika eneo hilo.

Wapalestina zaidi ya 41 elfu wameuawa shahidi na maelfu ya wengine kujeruhiwa tangu Israel ianzishe vita na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza mwezi Oktboba mwaka jana. 

Mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya wakazi wa Gaza 

 

Tags