Sep 14, 2024 04:24 UTC

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa iwapo Waislamu watashirikiana na kuwa kitu kimoja utawala wa Israel hautathubutu kufanya mauaji ya umati dhidi yao. Rais Masoud Pezeshkian ameeleza haya alipokutana na kuzungumza jana huko Basra Iraq na wasomi wa kitamaduni, kidini, kielimu na wengineo.

Akiwa katika marhala ya mwisho ya ziara yake rasmi ya siku tatu huko Iraq, Rais Masoud Pezeshkian jana Ijumaa baada ya kuwasili katika mji wa Basra, alikutana na kuzungumza na wasomi, wanafunzi wa vyuo vikuu na viongozi wa makabila ya Iraq na akasema katika hotuba yake kuwa: Imam Ali (a.s) hakusema kuwa waumini ni sawa na waumini wengine bali amesema' Muislamu ni sawa na Muislamu mwenzake na kwamba utawala wa Kizayuni kamwe hautathubutu kuwaua kwa umati Waislamu kama wote watashikamana na kuwa kitu kimoja. 

Rais Masoud Pezeshkian Jumatano iliyopita aliwasili Baghdad mji mkuu wa Iraq katika ziara yake ya kwanza nje ya nchi huku akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran na kulakiwa rasmi na Muhammad Shia al Sudani Waziri Mkuu wa Iraq. 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika siku mbili zilizopita mbali na kukutana na kuzungumza na Rais, Waziri Mkuu na viongozi wa eneo la Kurdistan la Iraq, alifanya ziara katika haram tukufu za Imam Ali (as) na  Imam Hussein (as) na kumzuru pia  Abul Fadhl Abbas (as).

Rais Pezeskhian baada ya kuwasili katika mji wa Karbala

Safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ujumbe aliofuatana nao huko Iraq imeakisiwa pakubwa katika vyombo vya habari vya Iraq na vya nchi nyingine duniani.