-
Bagheri Kani: Iran ina azma ya kuendeleza sera za ujirani za Ebrahim Raisi
Jun 24, 2024 22:59Mwakilishi maalumu wa Sultan wa Oman ambaye yuko hapa Tehran kushiriki katika mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia yaani Asia Cooperation Dialogue (ACD) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran pambizoni mwa mkutano huo.
-
Mokhber: ACD inaweza kuwa na mchango muhimu katika kuasisi Asia yenye umoja, nguvu na athirifu zaidi
Jun 24, 2024 08:00Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametuma ujumbe katika Jukwaa la Mazungumzo ya Ushirikiano wa Asia yaani Asia Cooperation Dialogue (ACD) la kundi la D-8 hapa njini Tehran kwamba Asia inaweza kuwa chanzo cha mabadiliko chanya katika michakato ya kimataifa na kichocheo kikubwa cha umoja na mshikamano wa kimataifa.
-
Iran yaalani mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Dagestan, Russia
Jun 24, 2024 07:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani mashambulizi ya kigaidi yaliyojiri katika Jamhuri ya Dagestan na kutoa mkono wa pole kwa taifa la Russia na serikali ya nchi hiyo khususan familia za wahanga wa jinai hiyo.
-
Makubaliano ya kuanzisha mazungumzo kati ya Tehran na Manama, ishara ya mafanikio ya siasa za nje za Iran
Jun 24, 2024 07:33Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja zikielezea kuwekwa mikakati muhimu ya kuanzisha mazungumzo baina ya nchi mbili kwa lengo la kuchunguza namna ya kurejesha uhusiano wa kisiasa. Taarifa hii ya pamoja imetolewa kufuatia mazungumzo yaliyofanyika karibuni kati ya Ali Bagheri Kani, Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri mwenzake wa Mashauri ya Kigeni wa Bahrain.
-
Iran, Bahrain zakubaliana kuanzisha mazungumzo ya kurejesha uhusiano wa kisiasa baina yao
Jun 24, 2024 03:46Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Bahrain zimetoa taarifa ya pamoja na kutangaza kuweko kwao tayari kuanza mazungumzo ya kutafuta njia za kurejesha uhusiano wao wa kisiasa na kidiplomasia.
-
Umuhimu wa safari za kampeni za wagombea wa uchaguzi wa rais wa Iran
Jun 24, 2024 03:19Siku ya Jumamosi, mikutano ya kampeni za uchaguzi za wagombea wa muhula wa 14 wa uchaguzi wa rais wa Iran ilifanyika katika miji tofauti humu nchini na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi.
-
Gharibabadi: Marekani si mkweli kwa wananchi wa Iran
Jun 23, 2024 23:08Katibu wa Baraza la Haki za Binadamu la Iran amesema kuwa, Marekani si mkweli kwa wananchi wa Iran.
-
Matarajio ya kimkakati ya Kiongozi Muadhamu kwa Vyombo vya Mahakama nchini
Jun 23, 2024 08:05Akizungumza jana Jumamosi katika hadhara ya viongozi wa Vyombo vya Mahakama nchini, Ayatullah Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza matarajio yake kutoka kwa muhimili huo wa dola.
-
Mgombea Urais: Iran haipaswi kujifunga katika mazungumzo na nchi chache tu
Jun 23, 2024 07:43Saeed Jalili, mgombea wa urais wa Iran unaotarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki hii ya Juni 28, amesema kuwa, Iran haipaswi kujifunga katika mazungumzo na nchi chache tu, bali inabidi kuwa wazi kwa nchi zote duniani.
-
Kiongozi Muadhamu asisitiza kupatiwa ufumbuzi matatizo ya wananchi kwa uadilifu
Jun 22, 2024 08:37Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kupatiwa ufumbuzi matatizo na hitilafu za wananchi kwa uadilifu na kujiepusha na kuvuka mstari mwekundu wa sheria ni kati ya majukumu makuu ya mhimili wa mahakama.