-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Iran haitasita kulinda maslahi yake
Apr 15, 2024 01:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita wala kuwa na shaka katika kulinda maslahi yake halali dhidi ya uchokozi wowote mpya.
-
Rais Raisi: Hatua yoyote ya kifidhuli itakabiliwa na jibu kali zaidi la Iran
Apr 14, 2024 07:42Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli utakabiliwa na jibu madhubuti, zito na kali zaidi.
-
Hatua ya kijeshi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni; mfano halisi wa "kujitetea halali"
Apr 14, 2024 07:10Katika kujibu shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alfajiri ya Jumapili ya leo tarehe 14 April 2024 imefanya mashambulizi ya moja kwa moja ya ndege zisizo na rubani na makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).
-
Kamanda wa IRGC: Iwapo Israeli itashambulia tena, itapokea jibu kubwa zaidi
Apr 14, 2024 04:26Kamanda mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameonya kwamba uvamizi wowote zaidi wa kijeshi utakaofanywa na utawala wa Israel utakabiliwa na jibu kubwa zaidi kutoka Iran.
-
Balozi wa Iran UN: Jibu la Iran litakuwa kali zaidi iwapo Israel itaanzisha tena mashambulizi
Apr 14, 2024 04:15Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa ametangaza katika barua kwa Baraza la Usalama kwamba ikiwa utawala wa Israel utaanzisha tena mashambulizi yoyote ya kijeshi, bila shaka jibu la Iran litakuwa la nguvu na kali zaidi.
-
Wananchi wa Iran, duniani wajitokeza mitaani kuunga mkono hatua ya IRGC kuiadhibu Israel
Apr 14, 2024 04:09Wananchi konte nchini Iran wamejitokeza mitaani kuunga mkono hatua ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ya kuuadhibu utawala wa Kizayuni wa Israel kufuatia kitendo chake cha kichokozi cha kutekeleza mashambilizi ya kigaidi dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran jijini Damascus Aprili Mosi.
-
IRGC yalipizia kisasi kwa mashambulizi 'makubwa' ya makombora na drone dhidi ya Israel
Apr 13, 2024 23:45Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limefanya mashambulizi makubwa ya kulipiza kisasi kwa kutumia makombora na ndege zisizo na rubani dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel likijibu mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa utawala wa Israel ya tarehe 1 Aprili dhidi ya majengo ya kidiplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu katika mji mkuu wa Syria, Damascus.
-
IRGC yaikamata meli yenye uhusiano na Israel katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Apr 13, 2024 09:26Shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kiisamu ya Iran IRNA limeripoti kuwa kikosi maalumu cha wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kimekamata meli ya makontena ya MCS Aries yenye uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.
-
Kuwa jadi Iran katika kujibu shambulio na kuongezeka harakati na mashauriano ya Wamagharibi
Apr 13, 2024 08:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amejibu simu alizopigiwa na Annalena Baerbock, David Cameron na Penny Wong Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Uingereza na Australia.
-
Iran yataka Italia ichukue hatua kukomesha mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina
Apr 13, 2024 04:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian ameitaka Italia kufanya juhudi za kukomesha mauaji ya kimbari na jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.