Jun 22, 2024 12:07 UTC
  • Kiongozi Muadhamu asisitiza kupatiwa ufumbuzi matatizo ya wananchi kwa uadilifu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa kupatiwa ufumbuzi matatizo na hitilafu za wananchi kwa uadilifu na kujiepusha na kuvuka mstari mwekundu wa sheria ni kati ya majukumu makuu ya mhimili wa mahakama.

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo amekutana na maafisa wa Idara ya Mahakama ya Iran na kusema: "Kutatua masuala na mizozo ya wananchi kwa kuzingatia haki na kuzuia kuvuka mstari mwekundu wa sheria ni miongoni mwa majukumu makuu ya mhimili  wa mahakama." Ameongeza kuwa, jukumu kuu zaidi la mhimili wa mahakama ni kutekeleza uadilifu kwa ujasiri na bila kuyumba. 

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu huku akisisitiza kuwa hakuna masuala ambayo yamepewa uzito mkubwa kama suala la 'uadilifu' katika Qur'ani Tukufu na vyanzo vingine vya Uislamu, amesema, ujasiri ni jambo la lazima kwa ajili ya kutekeleza uadilifu. Amesisitiza kwamba utoaji maamuzi ya mahakama unapasa kutegemea sheria za ndani ya nchi na si vyanzo vya haki za binadamu vya Magharibi, 

Ayatullah Khamenei 

Akiendelea na hotuba yake, Ayatullah Khamenei ameashiria kukaribia duru ya 14 ya uchaguzi wa Rais wa Iran; na katika nasaha zake muhimu kwa wagombea wa uchaguzi huo amesisitiza kuwa mijadala ya wagombea kwenye televisheni au matamshi yao sehemu nyingine yasisababishe mgombea mmoja kutamka maneno yanayowafurahisha maadui wa Mfumo wa Kiislamu, kwa ajili tu ya kutaka kumshinda mpinzani wake.