-
Rais Raisi: Operesheni ya "Ahadi ya Kweli" ilikuwa hatua ya kiwango maalumu na ya kuwatia adabu tu Wazayuni
Apr 17, 2024 07:41Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilikuwa hatua ya kiwango maalumu na ya kuutia adabu tu utawala wa Kizayuni na akasisitiza kwamba, endapo utawala huo utafanya uchokozi mdogo kabisa dhidi ya ardhi ya Iran utakabiliwa na jibu kali zaidi na la nguvu kubwa zaidi.
-
Iran iliwasiliana na nchi za eneo katika kutekeleza Operesheni ya Ahadi ya Kweli dhidi ya Israel
Apr 17, 2024 07:19Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na masuala ya kisiasa amesema: Iran ilikuwa ikiwasiliana na nchi za eneo katika mchakato wa kutoa jibu kwa utawala wa Kizayuni na utekelezaji wa Operesheni ya Ahadi ya Kweli.
-
Ebrahim Raisi: Wazayuni wataelewa maana halisi ya majibu ya Iran
Apr 17, 2024 03:18Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, iwapo Israel itafanya kosa jingine lolote dhidi ya Iran, basi Wazayuni na waungaji mkono wao wataelewa maana halisi ya majibu ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Amir-Abdollahian: Mgogoro wa Asia Magharibi umesababishwa na mashambulizi ya Israel
Apr 17, 2024 03:17Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amefanya mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan na kusisitiza kuwa, mgogoro uliopo katika eneo la Asia Magharibi hivi sasa umesababishwa na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza.
-
'Operesheni ya Ahadi ya Ukweli' ya Iran imesambaratisha dhana potofu ya kutoshindwa Israel
Apr 16, 2024 23:58Kamanda wa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Brigedia Jenerali Kioumars Haydari amesema operesheni ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel imeondoa zaidi dhana potofu kwamba utawala huo khabithi na muuaji watoto hauwezi kushindwa.
-
Grossi asisitiza tena kutokuwepo shughuli za kijeshi za nyuklia nchini Iran
Apr 16, 2024 22:58Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amesisitiza kuwa, hakuna nyaraka zozote zinazothibitisha utengenezaji wa silaha za nyuklia nchini Iran na kuwa, mivutano ya hivi sasa haijavuruga mchakato wa ufuatiliaji wa wakala huo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.
-
Ebrahim Raisi: Hatua yoyote dhidi ya Iran itapata majibu makali
Apr 16, 2024 07:19Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hatua yoyote hata ndogo kiasi gani itakayochukuliwa dhidi ya manufaa ya Iran, bila ya shaka yoyote itapata majibu makali na ya kuumiza kwa wote watakaohusika na hatua hiyo.
-
Amir-Abdollahian: Iran haitoruhusu Israel kuhatarisha usalama wa ukanda huu
Apr 16, 2024 07:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kwamba usalama na utulivu wa nchi za eneo hili zima ni muhimu sana kwake, bali ni sawa kabisa na usalama wake yenyewe na haitoruhusu utawala wa Kizayuni kuhatarisha usalama wa eneo hili kwa chokochoko zake.
-
Abdollahian amwambia Guterres: Hatukuwa na njia nyingine isipokuwa kuiadhibu Israel
Apr 16, 2024 03:38Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, operesheni ya jeshi la Iran dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala ghasibu wa Israel imefanyika ndani ya fremu ya kujilinda na kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
-
Tehran yaitaka UN ilaani shambulio la Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus
Apr 15, 2024 22:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina wajibu wa kulaani shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria.