-
Tehran yaitaka UN ilaani shambulio la Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus
Apr 15, 2024 22:45Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lina wajibu wa kulaani shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria.
-
Amir Abdollahian: Israel ikiendeleza chochoko itapewa kichapo kikubwa zaidi
Apr 15, 2024 10:16Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa uungaji mkono wa Ujerumani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na kusema kuwa, iwapo utawala wa Israel unataka kuendelea na chokochoko zake, majibu yake yatakuwa ya haraka na makubwa zaidi.
-
PressTV: Makombora yote ya hypersonic yaliyotumiwa na Iran dhidi ya Israel yalilenga shabaha + Video
Apr 15, 2024 10:15Makombora yote ya hypersonic yaliyotumiwa katika mashambulizi ya Iran ya kuiadhibu Israel yamepiga malengo yaliyokusudiwa baada ya kukwepa mifumo ya ulinzi ya anga ya utawala huo harami na washirika wake.
-
Onyo la Iran kwa Marekani na Magharibi kuhusu madhara yatakayozipata zikiiunga mkono Israel
Apr 15, 2024 08:32Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeionya na kuitahadharisha Marekani na nchi za Magharibi juu ya kuuunga mkono kijeshi utawala wa Kizayuni na kufanya chokochoko dhidi ya Iran na kutangaza kwamba, iwapo nchi hizo zitaingilia kati katika kuuunga mkono utawala wa Kizayuni, vituo vyao vyote na maeneo yote ya maslahi yao yatashambuliwa na vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Amir Abdollahian: Iran haikuwa na budi ila kuuadhibu utawala wa Kizayuni ndani ya fremu ya kujilinda halali
Apr 15, 2024 04:39Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haikuwa na budi ila kuutia adabu utawala wa Kizayuni katika fremu ya kujilinda halali kufuatia Umoja wa Mataifa kunyamaza kimya na kushindwa kuchukua hatua za kidplomasia huku Baraza la Usalama la umoja huo likishindwa hata kutoa tamko la kulaani shambulio la utawala wa Israel katika ubalozi mdogo wa Iran huko Syria.
-
Shehena ya mbolea ya kemikali iliyotengenezwa na utawala wa Kizayuni yakamatwa kaskazini magharibi mwa Iran
Apr 15, 2024 04:29idara ya Forodha ya Iran imetangaza kuwa imezuia shehena ya mbolea ya kemikali iliyotengenezwa katiika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) iliyokuwa ikisafirishwa huko kaskazini magharibi mwa Iran.
-
Iran yaionya tena Marekani dhidi ya kuchukua hatua za kijeshi
Apr 15, 2024 01:06Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameionya Marekani kuhusu kuanzisha hatua za kijeshi dhidi ya Iran baada ya operesheni yake ya kisheria ya hivi karibuni ya kulipiza kisasi dhidi ya utawala ghasibu wa Israel, mshirika mkuu wa kieneo wa Washington.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Iran haitasita kulinda maslahi yake
Apr 15, 2024 01:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita wala kuwa na shaka katika kulinda maslahi yake halali dhidi ya uchokozi wowote mpya.
-
Rais Raisi: Hatua yoyote ya kifidhuli itakabiliwa na jibu kali zaidi la Iran
Apr 14, 2024 07:42Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel utafanya harakati yoyote ya kifidhuli utakabiliwa na jibu madhubuti, zito na kali zaidi.
-
Hatua ya kijeshi ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni; mfano halisi wa "kujitetea halali"
Apr 14, 2024 07:10Katika kujibu shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus, mji mkuu wa Syria, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alfajiri ya Jumapili ya leo tarehe 14 April 2024 imefanya mashambulizi ya moja kwa moja ya ndege zisizo na rubani na makombora katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel).