Apr 15, 2024 07:59 UTC
  • Shehena ya mbolea ya kemikali iliyotengenezwa na utawala wa Kizayuni yakamatwa kaskazini magharibi mwa Iran

idara ya Forodha ya Iran imetangaza kuwa imezuia shehena ya mbolea ya kemikali iliyotengenezwa katiika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) iliyokuwa ikisafirishwa huko kaskazini magharibi mwa Iran.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, maafisa wa forodha wa ofisi ya forodha ya Bazargan wamezuia shehena hiyo ya mbolea ya kemikali yenye mada ya potasiamu nitrate iliyotengenezwa na utawala wa Kizayuni, ambayo ilikuwa imepakiwa kwenye lori kuelekea Uzbekistan. 

Kwa mujibu wa ripoti hii, ni marufuku kuingiza na kusafirisha bidhaa zozote zinazotengenezwa na utawala wa Kizayuni kupitia forodha za Iran, na hivi karibuni maafisa wa forodha wamekuwa wakifuatilia vikali usafirishaji wa bidhaa hizo.

Tags