Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Iran haitasita kulinda maslahi yake
(last modified Mon, 15 Apr 2024 04:30:40 GMT )
Apr 15, 2024 04:30 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Iran haitasita kulinda maslahi yake

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitasita wala kuwa na shaka katika kulinda maslahi yake halali dhidi ya uchokozi wowote mpya.

Baada ya shambulio la tarehe 1 Aprili lililofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika sehemu ya ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus, Syria kama sehemu ya ardhi ya Iran na kuwauwa shahidi washauri saba wa Iran waliokuwepo kisheria nchini Syria huku jamii ya kimataifa ikinyamazia kimya jinai hiyo; jana asubuhi Aprili 14 Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu kiliuadhibu utawala ghasibu wa Israel kwa kurusha ndege zisizo na rubani (droni) na makombora kadhaa kuelekea maeneo yanayokaliwa kwa mabavu. 

Amir Saeed Iravani Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa pia amesema kuwa Iran imetekeleza hatua hiyo ya kijeshi kwa mujibu wa kifungu cha 51 cha Hati ya Umoja wa Mataifa kuhusu kujilinda kihalali na kujibu hujuma za kijeshi za utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya kidiplomasia vya Iran huko Damascus.  

Amir Saeed Iravani 

Mkuu wa chombo cha sera za nje za Iran ameendelea kubainisha kuwa, hadi hapa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina nia ya kuendelea na operesheni za kujihami, lakini ikibidi haitosita kulinda maslahi yake halali dhidi ya uvamizi wowote mpya.

Tags