Apr 17, 2024 11:11 UTC
  • Rais Raisi: Operesheni ya

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilikuwa hatua ya kiwango maalumu na ya kuutia adabu tu utawala wa Kizayuni na akasisitiza kwamba, endapo utawala huo utafanya uchokozi mdogo kabisa dhidi ya ardhi ya Iran utakabiliwa na jibu kali zaidi na la nguvu kubwa zaidi.

Kwa mujibu wa IRNA, Rais Raisi ameyasema hayo leo asubuhi katika hafla ya gwaride la Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo sambamba na kutoa pongezi kwa mnasaba wa maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Iran amesema: "Jeshi liko pamoja na taifa la Iran na limejiweka tayari kikamilifu kwa ajili ya kulinda nchi, ardhi yote na tunu za Mapinduzi ya Kiislamu".
 
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: baada ya Kimbunga cha Al-Aqsa cha Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni, Operesheni ya Ahadi ya Kweli imeporomosha haiba ya utawala huo na kuthibitisha kuwa, nguvu zao ni za utando wa buibui tu; na nguvu na uwezo ambao Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na Jeshi zimeonyesha kulingana na amri iliyotolewa na Amiri Jeshi Mkuu ulikuwa ni wa kuutia adabu utawala wa Kizayuni.
Gwaride la maadhimisho ya Siku ya Jeshi la Iran

Sayyid Ebrahim Raisi ameongezea kwa kusema: "Operesheni ya Ahadi ya Kweli ilikuwa ya kiwango maalumu na si ya pande zote. Kama ingepangwa kuchukuliwa hatua kubwa, wangeona utawala wa Kizayuni usingesalia chochote, lakini ilipangwa iwe ni hatua ya kiwango maalumu, ya kuutia adabu utawala wa Kizayuni na kuvilenga vituo vilivyochukua hatua dhidi ya Iran".

 
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, utawala wa Kizayuni umeshindwa kiintelijensia, kiusalama, kijeshi na kimkakati na akabainisha kwamba: katika fasihi ya Wamarekani hakujazungumziwa kuwepo mezani chaguo la kijeshi na hilo limetokana na nguvu na uwezo wa vikosi vya ulinzi vya Iran.
 
Sambamba na kutangaza uungaji mkono kwa taifa la Palestina, Rais Raisi amezihutubu nchi za eneo akisema, vikosi vya majeshi ya Iran ni walinda usalama, waleta amani, ni sababu ya kulifanya eneo liwe na nguvu uwezo na ni vya kutegemewa kikamilifu; kwa hivyo badala ya nchi hizo kujenga uhusiano na utawala wa Kizayuni zitegemee uwezo wao wenyewe, nguvu za Waislamu, Jeshi na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; na hakuna haja ya kuwepo vikosi vya kigeni katika eneo".../

 

Tags