-
Kanani: Iran iko tayari kuandaa mazingira ya kufikiwa amani nchini Ukraine
Mar 13, 2023 22:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Tehran imekuwa ikipinga vita vya Ukraine tangu mwanzo, na kutangaza utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu wa kuandaa mazingira yanayofaa kwa ajili ya kufikiwa amani na kusimamishwa vita nchini Ukraine.
-
Rais Raisi: Iran iligeuza vitisho, vikwazo kuwa fursa ya kustawi
Mar 13, 2023 09:26Rais wa Iran Ebrahim Raisi amesema Jamhuri ya Kiislamu imegeuza vitisho vinavyotokana na vikwazo vya upande mmoja kuwa fursa ya kupata maendeleo makubwa.
-
Iran: Makubaliano yetu ya kubadilishana wafungwa na Marekani, yasitumiwe kisiasa
Mar 12, 2023 23:28Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, kwa mtazamo wa Jamhuri ya Kiislamu, makubaliano ya kubadilishana wafungwa ni suala la kibinadamu kikamilifu na halipaswi kugeuzwa kuwa uwanja wa tamthilia za kisiasa.
-
Wazayuni wahamakishwa na mapatano baina ya Iran na Saudia
Mar 12, 2023 04:43Makubaliano yaliyofikiwa siku ya Ijumaa ya mjini Beijing China kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia yalipokelewa kwa shangwe na nchi za eneo na kwingineko, lakini yamewahamakisha Wazayuni.
-
Iran yakosoa undumakuwili wa Ufaransa juu ya suala la haki za binadamu
Mar 12, 2023 04:29Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani undumakuwili wa Ufaransa, ambayo kwa upande mmoja inajinadi kuwa mbeba bendera ya kutetea haki za binadamu, lakini kwa upande wa mwngine inakanyaga haki hizo kwa vitendo.
-
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu yapongeza mapatano baina ya Iran na Saudia
Mar 11, 2023 23:27Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imepongeza mapatano ya kurejesha tena uhusiano wa kidiplomasia kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia na kueleza kuwa, hiyo ni hatua muhimu katika uga wa kuimarisha amani na uthabiti katika eneo la Asia Magharibi.
-
Kumalizika mkwamo wa miaka saba katika uhusiano wa Iran na Saudi Arabia
Mar 11, 2023 23:08Iran na Saudi Arabia zimekubaliana kuanzisha tena uhusiano kati ya pande mbili kwa upatanishi wa China baada ya mkwamo wa miaka saba.
-
Iravani: Jamii ya kimataifa inapaswa kuchukua hatua za kupambana na chuki dhidi ya Waislamu
Mar 11, 2023 09:45Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalaani vikali ukatili wowote dhidi ya watu kwa misingi ya imani na dini na kuesema: "Wakati umefika kwa jamii ya kimataifa kupambana na chuki dhidi ya Waislamu ambao ni sehemu muhimu ya watu wa dunia."
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Mataifa yanayopigania haki na uadilifu yazidi kujuana
Mar 11, 2023 04:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza katika salamu zake kwa mataifa yanayozungumza Kihispania juu ya kuzidi kujuana na kushirikiana mataifa yanayotetea haki na uadilifu.
-
Spika Qalibaf: Kurejeshwa uhusiano wa Iran na Saudia ni hatua muhimu kwa uthabiti wa eneo
Mar 10, 2023 23:22Mohammad Baqer Qalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema, kurejesha uhusiano na Saudi Arabia ni hatua muhimu katika mwelekeo wa uthabiti wa eneo na Ghuba ya Uajemi na kustawisha mashirikiano ya kikanda kisiasa na kiuchumi.